Na Hussein Stambuli, Morogoro.

Jeshi la polisi mkoani morogoro limewakamata na kuwashikilia watuhumiwa 8 walio jihusisha na tukio la kuchoma nyumba ya mfugaji kwa sababu ya migogoro ya wakulima na wafugaji sambamba na kufunga barabara kuu ya dar-es salamu –morogoro maeneo ya maseyu mikese katika kushinikiza kuachiwa kwa watuhumiwa waliokamatwa kwa kitendo hicho cha kuchoma nyumba.

Kamanda wa polisi mkoani hapa Wilbroad  Mutafungwa amesema chanzo cha mgogoro huo ni kutokana na wananchi siku ya jana tarehe 13,5,2019 kuvamia nyumba ya mfugaji aliyefahamika kwa jina la mbega sultani boy kwa kudaiwa kulisha mifugo kwenye mashamba ya wakulima kwa muda mrefu.
Ambapo wanakijiji hao wakaivamia nyumba yake na kuchoma moto jumla ya nyumba tano baada ya kumkosa mfugaji huyo anayedaiwa kwa muda huo kuwepo mahakamani kukabiliana na kesi nyingine zinazo mkabili za kulisha mifugo mazao ya wakulima na kusababisha nyumba hizo kuteketea vibaya huku wake wa 2 na watoto 19 akiwemo mtoto mmoja mlemavu wakinusurika kifo.

“kufuatia tukio hilo tumefanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa wane kwa kosa la kufanya fujo na kufunga barabara ambao ni ernest mkandula (25), machemba samiki (40), juma shabani (40) shaban ally (45) wakazi wa kijiji cha maseyu na misako mikali inaendelea katika kijiji hicho na tumefanikiwa kuyaondosha magogo yaliyokuwa yamewekwa barabara na safari zinaendelea. Amesema mutafungwa

Kamanda wa polisi akatoa wito kwa wananchi kutii sheria na kuacha kujichukulia sheria mkononi kwani husababisha kukosa haki zao za msingi kwa kujiingiza kwenye makosa mengine..
 Kamanda  wa polisi mkoani morogoro wilbroad Mutafungwa na watuhumiwa 8 walio jihusisha na tukio la kuchoma nyumba ya mfugaji sambamba na kufunga barabara kuu ya dar-es salamu –morogoro maeneo ya maseyu mikese
 magari yakiwa yamesimama kutokana na kufungwa barabara kuu ya dar-es salamu –morogoro maeneo ya maseyu mikese.
 watuhumiwa 8 walio jihusisha na tukio la kuchoma nyumba ya mfugaji sambamba na kufunga barabara kuu ya dar-es salamu –morogoro maeneo ya maseyu mikese
wilbroad mutafungwa kamada wa polisi mkoa wa morogoro, akizungumza na waandishi wa habari mkoani morogoro

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...