Anaandika Abdullatif Yunus, Michuzi TV - Bukoba.

Hatimae Mashindano ya Mpira wa Miguu yaliyozikutanisha Timu za waendesha Pikipiki Manispaa ya Bukoba, maarufu kama JPM BODABODA CUP 2019 - KAGERA, Yamehitimishwa Mei 25, 2019 katika Uwanja wa Nyasi bandia wa Kaitaba.

Michuano hiyo iliyobeba hisia za wanasoka pamoja na wadau mbalimbali, imeratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera, ikiwashirikisha baadhi ya wadau wachache likiwemo Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera Kitengo cha Usalama Barabarani.

Katika fainali iliyozikutanisha Timu za Rwabizi Fc na Kasoma Fc, iliyohudhuriwa na mashabiki wengi wapenda soka kutoka Viunga mbalimbali vya Manispaa ya Bukoba, Rwabizi FC wameibuka wababe kwa kuichachafya bao 5 - 1Timu ya Kasoma.

Baada ya Mchezo huo kukamilishwa na mwamuzi Ahmada Simba, Uongozi wa Mkoa pamoja na Timu ya Maandalizi chini ya RC Marco Gaguti, wakakabidhi zawadi kwa washindi na washiriki licha ya Kiongozi huyo kukabidhi hati za Mamilioni ya Mikopo kwa Vikundi sita vya Bodaboda kwa ajili ya kujiendeleza kiujasiliamali.

Miongoni mwa Zawadi zilizotolewa kwa washindi ni pamoja na pesa Taslimu Milioni 3 kwa mshindi wa kwanza, Milioni 2 mshindi wa pili, Milioni moja  mshindi wa 3, Laki 2 mbili mshindi wa Nne, laki 2 Mfungaji bora, laki 2 mchezaji bora ambae pia aliongezwa shilingi Laki moja kutoka kwa Balozi wa kampeni ya Nyumba ni Choo Mrisho Mpoto. Sambamba na Zawadi hizo Timu nyingine zilizoshiriki zimepewa kifuta jasho shilingi elfu 50, kwa kila Timu pamoja na Zawadi ya Mpira mmoja mmoja kutoka CCM Mkoa wa Kagera kupitia Umoja wa Vijana Karagwe Saccos (UVIKASA).
 Hatimae Kikombe kikakabidhiwa kwa Washindi wa Mashindano hayo Rwabizi Fc 
 Maafisa usalama barabarani wakileta mwali uwanjani
 Mgeni rasmi wa Fainali hizo RC Gaguti akikagua Timu akisindikizwa na Viongozi wengine, nyuma yake ni Msanii Mrisho Mpoto.
 Picha ya pamoja waamuzi pamoja na manahodha wa Timu zote mbili.
 Sehemu ya mashabiki wengi waliohudhuria, wakiendelea kufuatilia mtanange huo wa Fainali ya JPM CUP
 Chama cha Mapinduzi kikikabidhi Zawadi za Mipira kwa RC Gaguti wakati wa mapunziko ya Mchezo wa fainali
 Wachezaji wa Timu ya Rwabizi Fc wakishangilia moja wapo ya Magoli kwa mtindo wa kulala chali
 Pichani Mgeni rasmi RC Gaguti akikabidhi hati ya Mkopo wa Shilingi Milioni sita kwa Kikundi cha Boda boda kwa ajili ya kujiendeleza katika mradi wao.

 Moja kati ya shughuli pevu iliyokuwa ikiendelea uwanjani
 Timu za Rwabizi FC na Kasoma FC zikiwa uwanjani Kaitaba tayari kwa ukaguzi kabla ya kuanza Mchezo wao Fainali ya JPM Bodaboda Cup
 Pichani Msanii na Balozi wa Kampeni ya Nyumba ni Choo akikabidhi Zawadi yao kwa mchezaji bora Bensoni, Shilingi laki Moja, Tisheti kumi na Kanga Kumi.
 Kikosi cha Kasoma Fc kilichoingia Fainali na kuibuka nafasi ya pili katika mashindano
Wababe wa Mashindano ya JPM Cup Kikosi cha Rwabizi Fc

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...