Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila akinukuu baadhi ya maoni ya wadau katika kikao cha wadau wa msaada wa kisheria kwa Mikoa ya Nyanda za juu Kusini inayojumuisha mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya, Rukwa na Songwe, kulia kwake ni Msajili wa Mashirika na taasisi zinazotoa Msaada wa Kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Felista Joseph

Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila ameelekeza kuwa mpango kazi wa kuratibu taasisi na mashirika yanayotoa msaada wa kisheria kwa wananchi ukamailike haraka ili wananchi wapate huduma ya usaidizi wa kisheria kwa ufanisi.

Kafulila ametoa maelekezo hayo jana wakati akifungua kikao cha wadau wa msaada wa kisheria kwa Mikoa ya Nyanda za juu Kusini inayojumuisha mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya, Rukwa na Songwe

“Watu wengi wamepoteza haki zao kwa kutokujua sheria au kutokuwa na fedha za kumudu gharama za mawakili lakini serikali imetengeneza utaratibu wa kuratibu taasisi ambazo zinatoa msaada wa kisheria bila malipo ili wananchi wengi zaidi wasiojiweza waweze kupata msaada wa kisheria na wasikose haki zao”, amesema Kafulila.

Amesema kuwa mpango kazi wa kuziratibu taasisi zinazotoa msaada wa kisheria uwe unapimika na hasa uwe na lengo la kutoa elimu kwa wananchi ili wajue kuwa hata kama hawana fedha za kugharimia mawakili wa kuwatetea ili wapate haki zao au hawana elimu juu ya sheria mbalimbali, zipo taasisi ambazo zinatoa huduma hiyo bila malipo.

Naye Msajili wa Mashirika na taasisi zinazotoa Msaada wa Kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Felista Joseph amesema kuwa elimu kwa umma itapewa kipaumbele katika mpango kazi huo na ni jambo la msingi ili wananchi wafahamu uwepo wa taasisi hizo

“Katika wiki ya msaada wa kisheria tunatoa elimu kwa wananchi kupitia vipeperushi, radio mbalimbali, tunazungumza nao katika maeneo mbalimbali pia orodha ya taasisi hizo huwekwa katika maeneo yote muhimu ili wananchi wajue kuna taasisi ambazo hutoa msaada wa kisheria pale ambapo watakuwa na uhitaji”, amesema Joseph.

Kwa upande wake Mratibu wa shirika la Gender and Social Reform Steward Shiwuga amesema shirika lake limekuwa likipata vikwazo katika kutoa msaada wa kisheria bila gharama yoyote na pia baadhi ya watendaji wamekuwa hawatoi ushirikiano kwao.

“Wananchi wakisikia huduma ya msaada wa kisheria tunaitoa bure wengine haamini wamezoa kutozwa fedha lakini pia baadhi ya watendaji wamekuwa hawatoi ushirikiano kwetu lakini tunaendelea kuwaelimisha wananchi na watendaji na matokeo tunayaona kwa sasa angalau ushirikiano umeanza kuongezeka na wananchi wanakuja kupata msaada”, amesema Shiwuga. 

Msajili Msaidizi wa Taasisi za Msaada wa kisheria kwa Wilaya ya Ileje Rodrick Sengela ameeleza kuwa hapo awali taasisi hizo zilijiendesha bila kuratibiwa pia baadhi ya watu wasio waaminifu walikuwa wakiwarubuni wananchi na kuwatoza fedha nyingi pale wanapohitaji msaada wa kisheria lakini kwa sasa wananchi wataelimisha mahali sahihi pa kupata msaada wa kisheria bila malipo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...