Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Samweli Rweyemamu akitoa elimu ya shinikizo la juu la  damu kwa wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo ikiwa ni moja ya maadhimisho ya siku ya shinikizo la juu la damu Duniani.
 Afisa Lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Maria Semlongo akitoa elimu ya lishe bora kwa afya ya moyo kwa ndugu wa wagonjwa wanaotibiwa  katika taasisi hiyo ikiwa ni moja ya maadhimisho ya siku ya shinikizo la juu la damu Duniani. Katika kuadhimisha siku hiyo JKCI ilifanya upimaji kwa ndugu waliowasindikiza wagonjwa ambapo asilimia 39 walikutwa na shinikizo la juu la damu bila ya kujifahamu.
 Afisa Lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Husna Faraji akizungumza na mmoja wa mzazi ambaye mtoto wake anatibiwa katika Taasisi hiyo  kuhusu lishe bora kwa watoto wakati wa maadhimisho ya siku ya shinikizo la juu la damu Duniani iliyogfanyika leo Jijini Dar es Salaam. Katika kuadhimisha siku hiyo JKCI ilifanya upimaji kwa ndugu wanaosindikiza wagonjwa kwa kuwapima viashiria vya magonjwa ya moyoambavyo ni urefu, uzito na  shinikizo la damu.
 Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Regan Valerian akizungumza na ndugu wa mgonjwa anayetibiwa katika Taasisi hiyo  wakati wa maadhimisho ya siku ya shinikizo la juu la damu Duniani iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Katika kuadhimisha siku hiyo wagonjwa walipewa elimu na ndugu waliosindikiza  walifanyiwa vipimo vya viashiria vya magonjwa ya moyo bila malipo ambapo asilimia 39 walikutwa na shinikizo la juu la damu bila ya kufahamu kuwa wanalo.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Steven Charles akimpima urefu na uzito ndugu wa mgonjwa anayetibiwa katika Taasisi hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya shinikizo la juu la damu Duniani iliyofanyika  leo jijini Dar es Salaam. Picha na  JKCI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...