Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv
SHAHIDI wa Tatu katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi Tisa wa Chadema, ameieleza mahakama kuwa alimshuhudia Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe akichukua kipaza sauti  na kutoa tamko la kuwashinikiza  viongozi wenzie na wafuasi wa Chadema kuandamana kuelekea katika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kuchukua barua.

Shahidi huyo, E 6976 Koplo Rahimu Msangi, ameeleza hayo leo, Mei 15, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba wa  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati akitoa ushahidi wake dhidi ya viongozi hao.

Mbali na Mbowe washtakiwa wengine ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vincent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu na Naibu Katibu Mkuu Bara na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika.

Wengine ni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya, Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.

Akiongozwa na wakili wa serikali Wankyo Simoni, Koplo Msangi amedai,  Februari 16,2018 huko Mwananyamala, katika viwanja vya Bauibui ambapo Chadema walikuwa wakifanya mkutano wa Kampeni alimshuhudia Mbowe akichukua kipaza sauti hicho kutoka kwa aliyekuwa Mgombea wa Ubunge jimbo la kinondoni (hakumtaja jina) aliyekuwa amepanda jukwaani akinadi sera zake na kisha kuanza kutoa tamko hilo.

Akieleza tukio hilo, Koplo Msangi amesema, siku hiyo yeye akiwa na maaskari wengine walifika eneo hilola buibui baada ya kupata maelekezo kutoka kwa Inspekta Mohamed Ngereje kuwa wafike pale, na wakiwa pale waliwashuhudia viongozi wa Chadema wakitoa maneno yanayoashiria uvunjifu wa amani.

Koplo Msangi ameendelea kudai kuwa, mbowe baada ya kuwatangazia wanachama wake waandamane, alishuka chini na kushikana mikono na viongozi wenzake waliokuwepo eneo hilo na kuandamana wakipitia mbarabara ya Mwananyamala, Kinondoni Studio hadi barabara ya Kawawa huku wakiimba nyimbo ambazo maneno yake yalisikika 'hatuogopi, hatushikiki, tutaandamana hadi kieleweke', .

Amedai, wandamanaji walionekan kuwa na hasira nanwalikuwa wameshika mawe,marungu na chupa za maji ambapo walipofika eneo la Mkwajuni,polisi walitoa irani ya kuwataka watawanyike lakini walikaidi na badala yake waliwarushia polisi mawe,na marungu ambapo yeye alipigwa jiwe eneo la shingoni na baada ya hapo hakufahamu kilichoendelea na kujikuta yupo hospitali amelazwa.

Ameeleza kuwa, alilazwa katika Hospitali ya Polisi (barracks)  iliyopo barabara ya Kilwa na aliposhtuka alikumbuka kwamba alikuwa na silaha aina ya SMG ambayo wakati huo hakuwa nayo lakini alikuja kuelezwa na Inspekta Ngereji kuwa, silaha take ipo kituo cha polisi cha Osterbay

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...