Na Agness Francis, Michuzi Tv.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Kidao Wilfred pamoja na Mkurugenzi wa Mashindano TFF Salum Madadi wanatakiwa  kushiriki kwenye semina ya FIFA ya siku mbili huko nchini Malawi. 

Uongozi wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) umetanabaisha kuwa semina hiyo itakayofanyika Blantyre nchini  humo ambayo inatarajia kuanza leo  Mei 15 na kumalizika kesho Mei 16 mwaka huu itahusiana na miundo mbinu

Uongozi huo umesema kuwa Washiriki 34 kutoka nchi mbalimbali watashiriki katika semina hiyo inayosimamiwa na  FIFA, huku ajenda kubwa ikiwa ni masuala ya miundo mbinu ya uboreshaji wa viwanja vya  mpira wa miguu.

Mbali na Tanzania tu nchi nyingine kutoka barani Afrika  zimealikwa kuhudhuria mkutano huo wa FIFA.

"Nchi hizo ambazo ni Uganda,Seychelles,Sudan Kusini,Misri,Eswatini,Eritrea,
Gambia,Lesotho,Cape Verde,Liberia,Msumbiji,Somalia,Afrika Kusini na Wenyeji wao Malawi" umesema uongozi wa TFF.
Mtendaji mkuu wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania  (TFF)   Wilfred Kidao. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...