Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Kaimu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto Leo ameendelea na ziara yake ya kutembelea Maeneo ya Manispaa hiyo yaliyopatwa na Madhara kutokana na mvua zinazonyesha, ambapo leo ametembelea kata ya Kivule.

Akiwa katika ziara yake Kumbilamoto ametemebelea eneo lililoangukiwa na Ukuta pamoja na kuwatembelea wale wote waliopatwa na majanga kutokana na kuanguka kwa ukuta huo na kuwasihi wakazi wa Manispaa kuchukua tahadahari kabla ya kufanya ujenzi na kuepuka ujenzi holela.

Kumbilamoto mara baada ya kutembelea eneo hilo alikwenda mpaka kwenye barabara ya Kinzudi Mwanagati ambayo imeharibika na mvua hadi kushindwa kupitika kwa sasa.

Amesema kuwa licha ya barabara hiyo kuharibiwa na mvua lakini tayari Manispaa ilishatenga kiasi cha fedha Milioni 650 ambazo zitafanya ukarabati wa eneo hilo na kujenga daraja linalounganisha mitaa hiyo miwili ambayo inategemeana katika shughuli za Maendeleo.

Kumbilamoto alitoa wito kwa wakazi kuchukua tahadhari hasa katika kipindi hicho cha mvua zinazonyesha kwa Mamlaka ya hali ya hewa imetangaza kuendelea kuwepo kwa mvua kubwa mpaka Mei 30  mwaka huu
 Sehemu ya Nyumba ambayo imeangukiwa na Ukuta wa nyumba ya jirani kutokana madhara ya mvua zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam.
Kaimu  Meya Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akitoa pole kwa Majeruhi waliobomokewa na Ukuta katika eneo la Mzinga kata ya kitunda jijini Dar es Salaam
 Kaimu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akikagua Barabara iliyoharibiwa na Mvua, barabra hiyo inayounganisha kinzudi na Mwanagati katika kata ya kitunda hivyo Manispaa ya Ilala imetenga milioni 650 kukarabati njia hiyo
 Kaimu Meye wa Manispaa ya Ilala akiwa ameongozana na Diwani wa Kata ya Kitunda wakati wa kukagua uharibifu uliofanywa na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam
 Kaimu Meya wa Manispaa ya Ilala ,Omary Kumbilamoto akipita kwenye Daraja linalounganisha Kinzudi na Mwanagati ambalo limejengwa kwa mbao na magaogogo ya Minazi lakini Manispaa ya Ilala imetenga fedha Shilingi Milioni 650 kwa ajili ya kurekebisha daraja hilo.

 Kaimu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akiangalia eneo la Nyumba iliyoangukiwa na Ukuta kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam eneo la Mzinga Manispaa ya Ilala,ambapo watu wawili wamejeruhiwa katika majanga hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...