Na Editha Karlo,Michuzi TV -Kigoma

KITUO cha sheria na haki za binaadamu(LHRC)kimewataka wakazi wa Mkoa wa Kigoma kwa kushirikiana na serikali za mitaa kuunda vikosi vya ulinzi mitaani kwaajili ya kuwalinda wanawake wasifanyiwe ukatili wa kingono.

Mkurugenzi mtendaji wa LHRC Anna Henga ameyasema hayo kwenye ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo wasaidizi wa sheria na waangalizi wa haki za binaadamu kanda ya Magharibi.

Anna amesema pamoja kuundwa kwa vikosi hivyo vya ulinzi,lakini pia wanawake wanaofanyiwa vitendo hivyo nao wanapaswa kutoa taarifa katika vyombo vya usalama haraka pale wanapopatwa na tatizo.

"Hapa Kigoma kuna kitu wanaita tereza,yaani wanaume wanajipaka mafuta ya mawese afu wanawaingilia wanawake kingono kwa nguvu,wanapiga,wanawajeruhi,wanawaibia na wakiwashika wanateleza baada ya kujipaka hayo mafunzo,Nimefika Kigoma mwenyewe ili niweze kujionea mwenyewe maana awali nilikuwa nasikia tu hizi habari za tereza,lakini nimeamini hili jambo lipo na baadhi ya waathirika waliofanyiwa vitendo hivyo nimeongea nao naamini tukishirikiana hili jambo litaisha"Alisema

Alisema kitendo wanachofanyiwa baadhi ya wanawake wa Kigoma mjini hasa maeneo ya Mwanga na Katubuka cha kuingiliwa kinguvu kingono,kupigwa na kuibiwa mali zao ni kitendo kibaya mno na hakiwezi kuvumiliwa.

"Mimi kazi yangu kutetea wanawake na watoto,kwa hapa Kigoma hiki kitendo ni kibaya ninawaomba wanawake watakaofanyiwa vitendo hivyo vya ukatili na hao akina tereza kutoa taarifa mara moja kwenye vyombo vya usalama ili waweze kupata msaada ikiwemo kuwakamata na hao waalifu"alisema

Naye Ofisa mratibu wa masuala ya ulinzi na usalama kutoka LHRC Renatha Selemani alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo watetezi wa haki za binaadam baada ya kuona kuna hatari nyingi za kiusalama zinawakabili.

Zawadi Jacob mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo amesema wamekuwa wakikutana na changamoto mbalimbali ikiwemo ya jamii kutokujua sheria na haki zao,na kusema mafunzo hayo yatamsaidia katika kazi zake pamoja na kuelimisha jamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binaadamu(LHRC)Anna Henga akizungumza na Waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo wasaidizi wa sheria na waangalizi wa haki za binaadamu kanda ya Magharibi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...