Na Agness Francis, michuzi Tv. 

MABINGWA  wa Afrika Mashariki na kati Azam fc kesho watashuka dimbani kuvaana na wakatamiwa wa Morogoro Mtibwa Sugar katika mchezo wa 37  mzunguko wa pili Ligi soka Tanzania bara. 

Afisa habari na msemaji wa klabu ya Azam fc Jaffary Maganga amezungumza leo Jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa mtanange huo Utapigwa katika dimba la uwanja wa Azam Complex Chamazi majira ya saa mbili usiku. 

"Baada ya kupoteza mchezo wetu uliopita dhidi ya Simba kwa kutoka  suluhu ya bila kufungana sasa tunashuka tena dimbani kuwakaribisha  Mtibwa Sugar ambapo tunajua kuwa ni timu kongwe na yenye uzoefu iliyopo ligi kuu muda mrefu"amesema Jaffary. 

Maganga amesema kuwa mchezo huo utakuwa wa ushindani kwao hivyo wanahitaji kucheza kwa utulivu na nidhamu ya hali ya juu ili kuhakikisha wanashinda gemu hiyo. 

"Tunakumbuka mchezo wa kwanza Mtibwa walifanikiwa mutufunga mabao 2-0 Sasa na sisi tutapambana  kutafuta ushindi wa nyumbani ukizingatia walimu walipata nafasi nzuri ya kuweza kuandaa timu kwa muda mrefu"amesema Msemaji huyo. 

Aidha ameeleza kuwa kikosi chao hakina majeruhi wachezaji wote wako fiti wapo tayari kwa ajili ya kupambania ushindi mnono wa alama 3 wakiwa nyumbani.

Azam anashuka dimbani akiwa nafasi ya 3 alama 69 akiwa ameshacheza michezo 36,huku yanga wakiwa juu yao kwa alama 83 wakiwa na michezo sawa, ambapo wekundu wa msimbazi Simba akiwa kinara wa Ligi kuu soka Tanzania bara akiwa na alama 88 na michezo 35.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...