MSHAMBULIAJI na nyota wa klabu ya Yanga sc Heritier Makambo inasemekana kuna tetezi za sintofahamu kuwa ametimkia nchini Guinea ambapo amesaini kandarasi ya miaka 3 na klabu ya Horoya  Athletic inayocheza ligi kuu nchini humo kwa ada ya 230,000,000 za kitanzania. 

Kwa mujibu wa ukurasa wa Instagram wa Yanga  umesema kuwa Makambo mwenye  umri wa miaka 25 amesaini  mkataba wa kuitumikia klabu hiyo miaka 3 na kupewa nafasi  kubwa ya kufanya makubwa  kwenye ligi kuu ya nchi hiyo hasa baada ya kuonyesha mafanikio makubwa akiwa kwenye kikosi cha Yanga. 

Makambo aliebakiza mkataba mmoja wa kuitumikia Yanga  uliokuwa umalizike mwakani 2020.

Hata hivyo  mwenyekiti wa  klabu ya Yanga  Mshindo Msolla ameweka wazi kwa   taarifa hizo zinazoleta sintofahamu kwa kueleza kuwa mshambuliaji huyo aliondoka na kocha Mwinyi Zahera  Mwinyi nchini Guinea  kuonana na uongozi wa timu hiyo kwa ajili ya kufanya vipimo vya afya  na ambapo angefaulu vipimo hivyo alipaswa kurudi nchini kuja kufanya mazungumzo na uongozi. 

"Ni kweli Makambo aliondoka juzi na mwalimu Zahera  kuelekea nchini humo kwa ajili ya vipimo vya afya kwa klabu ya Horoya, hivyo basi tunawasubiri warudi tuitazame ofa yao kisha tufanye biashara"amesema Mwenyekiti huyo. 

Aidha Msolla amesisitiza  kuwa "hizo taarifa za kutambulishwa rasmi sizielewi ila mwalimu akirudi tutatizama ofa yao na kulingana na klabu nyingine nyingi  zinazomtaka mchezaji huyo kisha tufanye maamuzi"

Nyota  huyoa ambaye ni  raia wa Congo alisajiliwa na klabu ya Yanga  ya Tanzania akitokea  Fc Lupopo ya nchi kwao kwa dau lisilopungua milioni 60 za kitanzanzania.
Mshabuliaji Herieter Makambo akiwa katika uzi wa Horoya Athletic klabu ya Guinea na viongozi wa timu hiyo amabapo inasemekana ameshasaini mkataba wa miaka 3 na klabu hiyo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...