Serikali ya Marekani imeondoa kwa
muda vikwazo vya kibiashara ilivyoweka wiki iliyopita dhidi ya kampuni ya simu
ya China Huawei.
Hatua hiyo inayolenga kupunguza hali ya kuvurugwa
wateja wake wanaotumia simu za kampuni hiyo.
Mwasisi wa kampuni hiyo anayesema
kuwa Huawei ilikuwa imejiandaa kwa hatua ya Marekani.
Wizara ya Biashara ya Marekani
itairuhusu kampuni ya Huawei kununua bidhaa zinazotengenezwa Marekani kwa siku
nyingine 90 ili kudumisha mitandao iliyopo na kutoa programu tumishi mpya kwa
simu za sasa za Huawei.
Kampuni hiyo kubwa kabisa duniani ya
kutengeneza vifaa vya mawasiliano ya simu bado imezuiwa kununua vifaa kutoka
nchini Marekani vya kutengenezea bidhaa mpya bila idhini za leseni ambazo kuna
uwezekano kuwa zitakataliwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...