Na.Khadija seif ,Globu ya jamii

MSIMU wa pili wa mashindano  ya keki  yazinduliwa rasmi jijini Dar es salaam.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa  muandaaji wa mashindano hayo zena Sharif amesema washiriki wameimarika na kwa msimu huu wapili washiriki wamekuwa wengi.

"Msimu wa pili tumefanikiwa kupata takribani washiriki 40 ambao watashindana kupika keki na mmoja kati yao ataibuka mshindi"

Zena amesema mashindano yapo mengi lakini swala la keki huwa halipewi kipaumbele sana kutokana na lilivojengeka katika jamii na kutopewa thamani lakini hakuna sherehe inayokosa keki.

Aidha,amesema mbali na vitabu ambavyo alivizindua mwaka jana kwenye msimu wa kwanza wa mashindano hayo kwa msimu wa pili ataweza kuleta kitu cha tofauti ambacho kitaendelea kuwa kama chachu kwa vijana hususani wasichana wenye umri mdogo kujituma na kutumia kazi za mikono kuongeza kipato.

Mashindano hayo wameweza kumkutanisha na watu mbalimbali huku wahitaji wa keki kuwa wengi kutokana na ubora wa keki za washiriki hao.

Hata hivyo kwa mshindi wa kwanza msimu wa kwanza Alexander Alex ambae aliibuka mshindi kutokana na ubora wa keki zake amesema mashindano hayo ni muhimu vijana kujitokeza na kushiriki kikamilifu na kutochagua kazi za kufanya.

"Mashindano ya keki yamenifungulia wigo mpana wa wateja na kuhimarika zaidi na kujifunza njia za washiriki wenzangu ambao walishiriki "

Pia ametoa wito kwa vijana hasa wa kiume kutochagua kazi za kufanya kwani kupika keki hakuchagui jinsi kwani ni anaingiza kipato kupitia kazi hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...