Na Ahmed Mahmoud,Manyara

Mfanyabiashara ,Furaha Lazaro (52),amelilalamikia jeshi la Polisi Mkoani Manyara ,katika kituo kidogo cha Polisi ,Mererani wilayani Simanjro kwa kushikilia Mali zake za Dukani zenye thamani ya sh,mil.9 bila sababu za msingi kwa muda wa mwaka mmoja.

Akiongea na Vyombo vya habari Jana ,Lazaro ambaye ni Mkazi wa mji mdogo wa Marerani ,amelituhumu jeshi hilo kwa kushikilia Mali zake baada ya kumhisi anajihusisha kununua bidhaa ambazo ni zao la uhalifu jambo ambalo si kweli.

"Naendesha Duka langu kwa fedha za mkopo kama mjasiriamali mdogo sasa Polisi wanashikilia Mali zangu tangia mwaka jana bila sababu ya msingi ,nitalipa na nini mkopo "alilalamika mama huyo

Alifafanua kuwa septemba tisa,mwaka jana Polisi wa kituo cha Mererani,walivamia Duka lake na kukusanya bidhaa mbali mbali yakiwemo Magodoro 15,Jenereta,mitungi ya gesi,Sabufa,Ving'amuzi ,mataili na Rimu Magari na kuondoka navyo hadi kituo cha Polisi.

Kadhalika askari hao pia walimkamata mfanyabiashara huyo na kuondoka naye hadi kituo cha Polisi na kuwekwa mahabusu wakimtuhumu kununua na kuuza Mali za wizi.

Akiongeza kuwa akiwa mahabusu alikuwa kiteswa kwa kipigo na askari wa upelelezi wakimlazimisha kueleza Mali anazouza amekuwa akizipata wapi jambo ambalo alidai Mali hizo huzinunua kwa Wateja wake wanaomletea zikiwa na risiti ama barua kutoka kwa Afisa Mtendaji.

"Mimi ni mjasiriamali huwa nauza bidhaa chakafu kama Mabati ,Milango ,Mgodoro na huwa nanunua zikiwa na risiti ama barua kutokana kwa Mtendaji na si vya wizi kama ambavyo Polisi wanahisi" Alisema Mama huyo.

Alisema baada ya mateso na kipigo cha muda mrefu akiwa mahabusu askari hao waliamua kumfungulia kesi na kumpeleka mahakamani katika mahakamanya Mwanzo Wilayani simanjiro kwa kosa la kuhisiwa kuuza bidhaa za wizi ,hata hivyo kesi hiyo ilimalizika baada ya kukosekana ushahidi.

Baada ya kesi kumalizika alianza kufuatilia Mali zake kituo cha Polisi bila kurudishiwa huku Polisi wakiendelea kumzungusha wakidai kuwa bado wanaendelea kuchunguza wakisubiri watu kuja kutambua Mali walizoibiwa.

Kamanda wa Polisi Mkoani Manyara,Agustino Senga alipohojiwa juu ya madai hayo alisema kuwa mama huyo bado anakesi nyingine mahakamani inayohusiana na Mali hizo.

"Huyo mama amekuwa akinunua vitu vya wizi na baadhi ya bidhaa zake tunazo na zipo kwenye mikono salama asubiri tukamilishe uchunguzi ,tunasubiri watu waje kutambua Mali zao walizoibiwa,tukikamilisha tutamrudishia" Alisema kamanda senga.

Hata hivyo alimtaka mama huyo kuwa mtulivu na kuacha kuhangaika kuandika barua ngazi mbalimbali za juu kwani pindi Polisi watakapojiridhisha hahusiki na tuhuma hizo atarejeshewa Mali zake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...