Rais Mstaafu, Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, katika nafasi yake kama mjumbe wa taasisi ya kutokomeza malaria (End malaria Council) alialikwa kuwa mgeni rasmi katika kikao cha 20 cha mawaziri wa afya wa shirikisho la kiuchumi la nchi za Afrika magharibi - ECOWAS - mjini  Cotonou, Benin. 
Kikao hicho kiliendeshwa chini ya chombo maalum cha afya cha  ECOWAS kinachojulikana kama WAHO – (West African Health organization).  Mkutano huu ni mwendelezo wa kikao cha kikazi ambacho Mhe. Kikwete aliendesha Addis Ababa mwezi wa pili mwaka huu alipokutana na wakuu wa taasisi za kikanda za kiuchumi na sasa anaendelea kuongea na  mawaziri wa afya katika kanda hizo.

Akimkaribisha kuongea katika kikao hicho Prof. Stanley Okolo, Mkurugenzi mkuu wa WAHO, alimtambulisha Mhe. Kikwete kuwa ni mkereketwa wa masuala ya afya na mpiganaji katika azma ya kutokomeza malaria. Kwani akiwa kama Rais wa Tanzania aliweza kuanzisha chombo cha  viongozi wakuu wa Afrika wanaopambana na malaria ijulikanayo kama African Leaders Malaria Alliance (ALMA)  ambacho kinaendelea kufanya kazi vizuri barani Afrika.  Kwamba hata baada ya kustaafu Urais bado anayaendeleza mapambano hayo kwa kupitia taasisi ya kutokomeza malaria ambapo yeye ni mjumbe. Taasisi ya kutokomeza malaria imeanzishwa na Bill gates na Ray Chambers na ina jumla ya wajumbe kumi na moja.  Mhe. Kikwete alikutana na mawaziri hao kwa nia ya kwanza kuwaelezea waheshimiwa uwepo wa taasisi ya kutokomeza malaria, pia kuwasisitizia kuhusu umuhimu wa kuongeza nguvu katika vita dhidi ya malaria.  

Katika Hotuba yake Mhe. Kikwete alielezea kuhusu tatizo la malaria duniani na azma ya Taasisi ya Kutokoeza Malaria kuhakikisha kuwa malaria inatoweka duniani kote.  Mhe. Kikwete alisema kuwa pamoja na mafanikio mazuri yaliyopatikana wakati ya mwaka 2000 hadi 2015 ambapo malengo ya millenia ya kupunguza wagonjwa navifo vya malaria yalitimia, report ya malaria ya mwaka 2018 inaonesha kuwa mafanikio hayo yamesimama na kwamba katika mwaka 2017, Asilimia 90 ya wagonjwa na vifo vya malaria vya dunia nzima vilitokea Afrika.  Report hiyo pia imebainisha kuwa nchi 11 zinabeba asilimia 80 ya wagonjwa na vifo vya malaria.  Ukiachia India nchi nyingine kumi zipo Africa ambazo ni Nigeria, Burkina Faso, Ghana, Niger, Mali, Cameroon, DRC, Mozambique, Uganda na Tanzania;  na tano kati ya hizi zipo Afrika Magharibi. Nchi za ECOWAS bado zilibeba karibia nusu ya wagonjwa na vifo vya malaria vya dunia. Pamoja na kuwa hizi nchi kumi zinabeba asilimia kubwa ya malaria katika Afrika, hali ya malaria pia si nzuri katika nchi nyinginezo.
Malaria ni ugonjwa ambao unaweza kutokomezwa kabisa hapa duniani, alielezea Mhe. Kikwete. Marekani ilitokomeza malaria mwaka 1956, China ambayo nayo ilikuwa na tatizo kubwa la malaria,  katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo haijakuwa na mgonjwa hata mmoja wa malaria na hapo Africa magharibi nchi ya Cabo Verde ipo katika mwelekeo wa kuondokana na malaria wakati Gambia na kaskazini mwa Senegal nao wapo kwenye hatua nzuri.  Hivyo ni vyema tukajifunza pia kutoka kwao.  Mheshimiwa Kikwete alisisitiza kuwa ni lazima juhudi za dhati ziwekwe ikiwa ni pamoja na uongozi wa juu wa serikali na wakuu wa Nchi kuwa mstari wa mbele katika mapambano. Uongozi thabiti wa program za malaria, ushirikiano katika kanda zetu, ili kuondokana na ugonjwa huu ambao sio tu ni tatizo la kiafya bali ni tatizo la kimaendeleo na ni lazima kila sekta nayo ijue kuwa inayojukumu katika vita hivi dhidi ya malaria.
 Rais Mstaafu Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, katika nafasi yake kama mjumbe wa taasisi ya kutokomeza malaria (End malaria Council) akiwa mgeni rasmi katika kikao cha 20 cha mawaziri wa afya wa shirikisho la kiuchumi la nchi za Afrika magharibi - ECOWAS- Cotonou, Benin. 3rd May 2018
  Rais Mstaafu Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, katika nafasi yake kama mjumbe wa taasisi ya kutokomeza malaria (End malaria Council) akihutubia katika kikao cha 20 cha mawaziri wa afya wa shirikisho la kiuchumi la nchi za Afrika magharibi - ECOWAS - Cotonou, Benin. 3rd May 2018
 Wajumbe wakimsikiliza  Rais Mstaafu Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, katika nafasi yake kama mjumbe wa taasisi ya kutokomeza malaria (End malaria Council) katika kikao cha 20 cha mawaziri wa afya wa shirikisho la kiuchumi la nchi za Afrika magharibi - ECOWAS - Cotonou, Benin. 3rd May 2018
 Rais Mstaafu Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, katika nafasi yake kama mjumbe wa taasisi ya kutokomeza malaria (End malaria Council) akhutubia katika kikao cha 20 cha mawaziri wa afya wa shirikisho la kiuchumi la nchi za Afrika magharibi - ECOWAS - Cotonou, Benin. 3rd May 2018

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...