Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo Kata ya Iyela (WDC) Jijini Mbeya wamehoji Ofisi ya afisa Mtendaji Kata hiyo juu Matumizi ya Fedha kiasi cha Shilingi Milioni 10 namna ambavyo zimetumika katika ujenzi wa Vyoo katika Shule ya Msingi Mapambano jijini Mbeya .

Aidha wameitaka Ofisi hiyo kutoa Maelezo ya Kina juu ya kusuasua kwa ujenzi wa vyoo hivyo ambao umedumu kwa zaidi ya mwaka mmoja licha ya kutolewa fedha hizo kutoka Halmashauri ya Jiji kupitia Mfuko wa Jimbo na michango ya Wananchi wakiwemo wadau wa maendeleo.

Hatua hiyo inakuja mara baada Wananchi wa Kata ya Iyela pamoja na wadau mbalimbali wanao unga mkono juhudi za Maendeleo katika Kata hiyo kuhoji juu ya Maendeleo ya ujenzi wa Vyoo kuchukua muda mrefu zaidi ya Mwaka mmoja licha Fedha kutolewa.

Akizingumza katika kikao cha Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo (WDC) Kata ya Iyela Mwenyekiti wa Shule ya Mapambano George Gidion amesema Wanafunzi wamekuwa wakipata adha kubwa kutokana na kuto kamilika kwa ujenzi wa vyoo hivyo hali ambayo ineleta hofu kwa afya za wanafunzi.

“Ujenzi wa vyoo hivi ni changamoto kubwa sana na tatizo kubwa lipo kwa Kamati ya Ujenzi pamoja na Ofisi ya Mtendaji kwani fedha ya ujenzi ilikwisha tolewa Shilingi mil 10 pamoja wadau mbalimbali kuchangia akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila,Naibu Spika Dkt .Tulia Ackson pamoja na Ndele Mwanselela Mdau wa Maendeleo.”Amesema Mwenyekiti huyo .

Naye Paul Mwangwiki Mwenyekiti wa Iyela 2

amesema kuna dalili kubwa ya ufisadi katika ujenzi wa vyoo hivyo kwani hata vifaa vya ujenzi vinavyotumika kuwa na uchakavu hivyo ametaka serikali ingilie Kati ili kuchunguza suala hilo.

Kwa upande wake mmoja wa wadau wa Maendeleo ambao wametoa mchango wao katika ujenzi wa Vyoo hivyo Ndele Mwanselela amesema kwa asilimia kubwa lawama zinatakiwa ziende kwa Mwenyekiti wa Mtaa huo pamoja na Kamati nzima ya Ujenzi kwani wao ndio wasimamizi wakubwa wa Mradi huo.

“Kinacho onekana hapa nikwamba ofisi ya Afisa mtendaji na Mwenyekiti wa Mtaa huu hakuna Mawasiliano kwasababu kila mmoja anaonesha kutolifahamu suala hili wakati wao ndio wasimamizi wakubwa wa mradi huu ,lakini Mimi kama Mdau wa maendelo siwezi lifumbia macho suala hili lazima hatua zichukuliwe kama itabainika kuna ufisadi.”Amesema Ndele Mwanselela.

Akizungungumzia hali hiyo Afisa Elimu Kata ya Iyela Dickson Sinkwembe amesema Fedha za ujenzi zilitolewa kwa kufuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na kutangaza zabuni kwa ajili ya kumpata Mkandarasi hivyo kusuasua kwa ujenzi huo kunatokana na usimamizi mbovu kwa Kamati ya Ujenzi .

Ujenzi wa Choo hicho umeanza toka 2018 ambapo Halmashauri kupitia mfuko wa jimbo walitoa kiasi cha Shilingi Milioni 10 pamoja na wadau mbalimbali kuchangia ujenzi wa vyoo hivyo ambapo Zaidi ya wanafunzi Mia900 Shule ya Msingi Mapambano wanategemea vyoo hivyo .

 Vyoo vya shule ya Msingi Mapambano Kata ya Iyela Jijini Mbeya ambao Ujenzi wake unadaiwa kuchukua muda mrefu pamoja na kutumia Shilingi Mil10
 Mdau wa Maendeleo Jijini Mbeya Ndele Mwaselela akichangia jambo Mbele ya wajumbe wa Kamati ya Maendeleleo Kata ya Iyela Jijini (Hawapo ) ambao waliketi kujadili maendeleo ya Ujenzi wa vyoo vya Shule ya Msingi Mapambano Jijini Mbeya .
 Afisa Elimu Kata ya Iyela Mbeya Dickson Simkwembe akizungumza katika Kikao cha Cha Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo Jijini Mbeya kilicho Keti Leo Mei 18 ,2019 katika Ukumbi wa Shule ya Msingi Mapambano.
George Gidioni Mwenyekiti wa Shule ya Msingi Mapambano jijini Mbeya akizungungumza katika Kikao cha Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo (WDC) Kata ya Iyela Leo  Mei 18 katika Shule ya Msingi Mapambano Jijini Mbeya .
 Wajumbe wa Mkutano

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...