Mkurugenzi wa wilaya ya Ileje Haji Mnasi akishiriki ujenzi na upanuzi wa hospitali ya wilaya ya ileje akiwa sambamba na mafundi wengine
 Mkurugenzi wa wilaya ya Ileje Haji Mnasi akishiriki ujenzi na upanuzi wa hospitali ya wilaya ya ileje akiwa sambamba na mafundi wengine

NA FREDY MGUNDA,ILEJE

MKURUGENZI wa wilaya ya Ileje Haji Mnasi ameshiriki ujenzi na upanuzi wa hospitali ya wilaya ya ileje baada ya kupokea kisai cha shilingi bilioni 1.5 kutoka serikalini ili kuhakikisha hospitali hiyo inajengwa kwenye ubora unaotakiwa na wananchi wanapata huduma bora za kiafya.

Akizungumza wakati wa ujenzi huo Mnasi alisema kuwa lengo la kushiriki ujenzi huo ni kuhakikisha anaweka hamasa kwa mafundi na wananchi kusimamia vilivyo kuhakikisha hospitali hiyo inajengwa kwa kiwango kinachotakiwa na serikali kuu.

“Mimi kama kiongozi lazima niwe mfano wa kuigwa kwa kufanya kazi kwa vitendo hivyo kuja kwangu kushiriki ujenzi huu ni kuonyesha jinsi gani tunatakiwa kufanya kazi tuliyoagizwa na Rais wetu” alisema Mnasi

Mnasi  alisema kuwa atahakikisha bega kwa bega katika usimamizi na ushiriki wa karibu kuhakikisha ujenzi unakamilika  na thamani ya fedha(value for money) kwa wakati ili kutimiza malengo ya serikali yanayokusudiwa.

“Nikija mara kwa mara kuangalia ujenzi huu nitahakikisha ujenzi ulio bora wa kuzingatia ujenzi unaofaata hatua zote za msingi na kupata majengo yaliyobora ya hospitali hii ya wilaya” alisema Mnasi

Lakini pia mkurugenzi Haji Mnasi aliishukuru na kuipongeza serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr John Pombe Magufuli kwa kuwajali wananchi kwa kutoa kiasi hicho cha pesa kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo ya wilaya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...