Wajumbe wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) wakifatilia mada mbalimbali zinazoendelea kuwasilishwa na wakufunzi kutoka nyanja tofauti katika siku ya kwanza ya Mkutano wao wa saba, unaofanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC, jijini Arusha. Kauli mbiu: 'Tutumie muda wetu vizuri kufanyakazi kwa ufanisi na kuleta tija kazini'.
Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), Zuhura Maganga akizungumza jambo katika siku ya kwanza ya Mkutano Mkuu Chama hicho, ulioanza leo kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC, jijini Arusha. 
Mhadhiri wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Charles George Magaya akizungumza wakati akiwasilisha mada ya umuhimu wa "Katibu Mahsusi kutunza siri na mzalendo katika kazi na Taifa kwa ujumla" wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), ulioanza leo kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC, jijini Arusha. 
Wakili wa Serikali, Berious Nyasebwa akizungumza wakati akiwasilisha mada yake iliyoelezea "Umuhimu wa Haki za Binadamu na Utawala Bora" wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), ulioanza leo kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC, jijini Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...