Na Editha Edward-Michuzi TV,Tabora 

Wizara ya Elimu, sayansi na teknolojia imesema inaendelea kuweka mikakati itakayosaidia Kukabiliana na Changamoto mbalimbali zinazowakabili wanafunzi wenye mahitaji maalumu wakiwemo Viziwi ili waweze kupata haki ya msingi ya Elimu sawa na watu Wengine

Yamebainishwa hayo na naibu katibu Mkuu wa wizara ya Elimu sayansi na teknolojia katika semina maalumu ya kujadili Changamoto mbalimbali zinazowakabili Viziwi iliyoandaliwa na chuo Kikuu cha Askofu Mkuu MIHAYO mjini Tabora

Akizungumza katika semina hiyo naibu katibu Mkuu Wizara ya Elimu sayansi na teknolojia anayeshughulikia Elimu msingi Dk. Evamaria Semakavu amesema kuna haja ya kuweka mazingira wezeshi kwa wenye Ulemavu hasa Viziwi 

"Wapo maprofesa wasioona Lakini inapofika kwa Viziwi Tanzania bado kuna Changamoto na sisi kama wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Tanzania ambao tumepewa jukumu la kusimamia suala la sera viwango na Mustakabali mzima na Sekta ya Elimu bado tunasema uziwi bado ni tatizo inapokuja kwenye Elimu ambapo tunahitaji kukusanya wadau wote ili kufanikisha hili"Amesema Dk. Semakavu

Paul Luzoka ambae ni Askofu Mkuu wa Jimbo kuu Catholic Tabora amesema anaomba serikali iongeze juhudi katika kuhakikisha inawajali kipekee zaidi Watoto wenye Ulemavu wa Kusikia

Aidha mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amesema watu wa Tabora wanatakiwa kumshukuru Mungu kwa kuona kuwa wadau wa Elimu kwa pamoja wanakubali kuweka mazingira wezeshi kwa watu wenye mahitaji maalumu 

Hata hivyo Muamko wa Elimu kwa Viziwi Mkoani Tabora bado upo chini ni jukumu la wazazi, Wadau wa Elimu na jamii kwa kuona umuhimu wa kuwasaidia watu hao wenye mahitaji maalumu ili kuwawezesha kuzifikiri ndoto zao.
 Ni mmoja kati ya watu wenye mahitaji maalumu akifuatilia jambo wakati wa mkutano.
Pichani ni naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dk. Evamaria Semakavu akizungumza na wadau katika semina Maalumu ya kujadili changamoto zinazowakabili Viziwi.

 Pichani ni wadau wa mkutano wa Elimu kutoka Sekta mbalimbali ndani na nje ya nchi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...