Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepokea msaada wa mashine za kutoa tiba ya saratani ya macho kwa watoto bila kuyaondoa zenye thamani ya shilingi milioni 170 kutoka Rotary Club Oyster bay jijini Dar es Salaam.

Msaada huu utawanufaisha watoto wengi wanaofikishwa hapa Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa huduma ya saratani ya macho kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa msaada, Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru ameishukuru Rotary Club kwa kuwa vifaa hivi vitatoa tiba sahihi kwa watoto mwenye saratani ya macho bila kufanyiwa upasuaji wa kuyaondoa.

Prof. Museru amesema watoto wenye seratani ya macho watakuwa wakipatiwa huduma ya mionzi baridi na moto.

“Huu ni msaada mkubwa kwani vifaa vitasaidia kutoa tiba sahihi kwa watoto wenye matatizo ya saratani ya macho. Muhimbili tuna zaidi ya watoto 100 wanaougua saratani mbalimbali, hivyo tuna kazi kubwa ya kuwapatia huduma bora ya afya,” amesema Prof. Museru.

Pia, Mkurugenzi ameipongeza shirika lisilo la kiserikali la Tumaini la Maisha Tanzania (TLM) kwa kutoa huduma bure ya matibabu,malazi na chakula kwa watoto wenye saratani ya aina mbalimbali.

Mkurugenzi wa Mradi wa Rotary Club ya Oyster bay, Kripa amesema wametoa msaada kwa ajili ya kuboresha huduma ya matibabu kwa watoto wenye saratani ya macho.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Macho, Dkt. Anna Sanyiwa wa Muhimbili amesema vifaa hivi ni vya kisasa na kwamba vinatumiwa na nchi mbalimbali duniani kutoa tiba ya saratani ya macho.

“Ni vifaa muhimu kwa tiba ya saratani ya jicho. Vifaa hivi vinatusaidia kuondoa vivimbe kwenye macho au jicho bila kufanya upasuaji wa kuondoa jicho la mgonjwa mwenye saratani. Kabla ya kupata vifaa, tulikuwa tunalazimika kuondoa jicho kwa mgonjwa,” amefafanua Dkt. Anna.

Amesema endapo watoto wenye saratani ya macho wakifikishwa hospitali mapema watatibiwa bila macho au jicho kuondolewa kwa kutumia vifaa vilivyokabidhiwa leo. Vifaa vilivyopokelewa leo ni mashini mbili ya mionzi ya moto, mashini moja ya mionzi baridi na kamera mbili.
 Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akizungumza baada kupokea msaada wa vifaa vinavyotumika kutoa huduma ya saratani ya macho kutoka Rotary Club Oyster bay jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto kwake ni  Rais wa Rotary Club Oyster bay ya Dar es Salaam, Vikash Shah na Mkurugenzi wa Mradi, Kripa. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa Muhimbili, Dkt. Baruani Sufiani na Dkt. Anna Sanjiwa wa Muhimbili.
 Prof. Lawrence Museru akikabidhiwa bango leo na Rais wa Rotary Club Oyster bay jijini Dar es Salaam, Vikash Shah.
 Prof. Museru wa Muhimbili na Rais wa Rotary Club, Vikash Shah wakiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa MNH na wawakilishi wa Rotary Club ya Oyster bay jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...