Na Ripota wetu, MICHUZI TV

MWILI wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dkt. Reginald Mengi utawasili nchini Jumatatu ya Mei 6, 2019 na ndege ya Shirika la ndege la Emirate ukitokea Dubai, Falme za Kiarabu.

 Mwanasheria wa familia ya Dkt. Mengi, Michael Ngalo amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mei 3, 2019 kuwa mwili wa Dkt. Mengi ambaye alifariki dunia akiwa huko Dubai usiku wa kuamkia Mei 2, 2019, ukishawasili jijini Dar es Salaam, utahifadhiwa kwenye hospitali Kuu ya Jeshi, Lugalo na siku inayofuata yaani Jumanne Mei 7, 2019, shughuli ya kuaga mwili huo itafanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar. 

Amesema kuwa baada ya shughuli hiyo ya kutoa salamu za mwisho, mwili wa Dkt. Mengi utasafirishwa Jumatano Mei 8, 2019 kuelekea mahala alikozaliwa Machame, Mkoani Kilimanjaro ambapo shughuli za mazishi zitafanyika Alhamisi Mei 9, 2019.

Wakati mwili wa Mengi ukisubiriwa kuwasili nchini maelfu ya watanzania wameendelea kutoa salamu za pole kwa familia yake huku viongozi na watu mashuhuri wakiwamo mabalozi wa nchi mbalimbali nao wameonesha kusikitishwa na kifo cha mzee Mengi.

Michuzi Blog na Michuzi TV zitaendelea kukujuza hatua hatua kinachoendelea kwa sasa nyumbani kwa Mengi wakati mwili ukisubiriwa kuwasili nchini Jumatatu jijini Dar es Salaam kabla ya kupelekwa mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...