SPIKA wa Bunge Mhe. Job Ndugai, amesitisha uwakilishi wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika, Mhe. Stephen Masele katika bunge hilo kuanzia leo Mei 16, 2019.

Sababu za hatua hiyo, Mhe. Ndugai amesema ni kutokana na utovu mkubwa wa kinidhamu ulioonyeshwa na Mhe. Masele ikiwemo kukaidi kurejea nyumbani kutokana na vitendo hivyo ili ahojiwe na Kamati ya Bunge ya Haki maadili na madaraka ya bunge.

Kwa sasa Mhe. Masele yuko nchini Afrika Kusini akiongoza vikao vya bunge la Afrika (PAP).

Akitoa taarifa ya Spika bungeni jijini Dodoma leo Mei 16, 2019, Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai aliliambia bunge kuwa, “Kuna matatizo makubwa sana ya kinidhamu yanayofanywa na Mhe. Stephene Masele, tuliagiza arudi nyumbani kuanzia Jumatatu iliyopita lakini amegoma, hata jana clips zinaonyesha akihutubia bunge la PAP japo ameitwa na spika lakini amedai kuwa ameagizwa na Waziri Mkuu aendelee (akakaidi) wito wa spika aendelee tu na mambo yake kule kitu ambacho ni uongo na kudhalilisha nchi,” Alisema Spika Ndugai, na kuendelea.

“Ni kiongozi ambaye amekuwa akifanya mambo ya hovyo hovyo ndio maana tumemuita ili ahudhurie kwenye kamati ya maadili atufafanulie huenda yuko sahihi lakini kwa mtazamo wetu amekuwa akifanya mambo ambayo ni hatari kubwa ikiwemo kugonganisha mihimili amekuwa akipeleka kwenye mhimili wa serikali juu kabisa maneno mengi ya uongo na ushahidi upo, kulidhalilisha bunge, ni kiongozi ambaye amejisahau hajui hata anatafuta kitu gani.” Alisema Spika Ndugai.

“Sasa kwakuwa tumekuwa tukimuita tangu Jumatatu na hataki kurudi ningependa kulifahamisha bunge hili kwamba kwa niaba yenu na mamlaka niliyonayo basi nimemuandikia barua Rais wa PAP ya kusitisha uwakilishi tuliompatia Mhe. Masele katika bunge la PAP hadi hapo kamati ya haki maadili na madaraka ya bunge itakapokamilisha uchunguzi dhidi yake na kukamilisha taarifa yake, kwahiyo kwamuda temporarily suspension ya Mhe. Masele kuwa mbunge wa bunge la Afrika hadi hapo tutakapomalizana naye hapa.” Alifafanua Spika Ndugai.

Pichani shoto ni SPIKA wa Bunge Mhe. Job Ndugai akipeana mkono na aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika, Mhe. Stephen Masele.kwa hisani ya K-VIS BLOG

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...