Na.Khadija seif,Globu ya jamii

RAIS wa muziki wa dance nchini Nyoshi El Sadat anatamani kufanya kazi na msanii wa bongofleva Nasib Abdul a.k.a Diamond.

Nyoshi amempongeza Diamond baada ya kuachia ngoma yake mpya "inama" aliomshirikisha msanii kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo Fally Ipupa na kupokelewa vizuri na mashabiki wa Kongo.

"Diamond ni mwanamuziki mkubwa kama mimi na ana uwezo mkubwa wa kufanya kazi na msanii yoyote yule nitamtafuta ili tufanye kazi pamoja,"

Nyoshi ameweka wazi hayo alipokuwa akizungumza na Globu ya Jamii,ameongeza kusema kuwa wanamuziki wote ni vizuri kushirikiana katika kazi bila kujali upande mmoja hasa likitokea swala la matamasha na kushirikishana kwenye wimbo.

"Likija swala la matamasha wanamuziki wa bongofleva wanaonekana peke yao ,sio vibaya wanamuziki wa dance wakashirikishwa ili kusiwepo tafsiri ya ubaguzi wa aina yoyote ile,"
 
Akifafanua zaidi katika lafudhi yake ile ile ya Kikongo,licha ya kuishi nchini kwa miaka mingi,Nyoshi amegusia swala la mavazi Kwa msanii ni moja ya kivutio Kwa mashabiki hata kama inatokea msanii haeleweki anachokiimba lakini muonekano wake unachukua nafasi mkubwa Kwa kile anachokifanya.

"Jux,daimond ,Irene uwoya, jackline wolper wanavaa vizuri nawapenda ", alisema nyoshi

Hata hivyo Nyoshi amesema muziki wa live bado upo na mashabiki wake bado wapo, Ila kwa sasa ndio unarudi kutokana na kipindi cha mwanzo kutengewa muda wa kufunga kumbi za starehe zinazopiga miziki, hasa ikifika saa 6 usiku na kupelekea kukosa mashabiki wengi.

"Mkuu wa mkoa amesikia kilio chetu kwani muziki ni ajira na tunatafuta riziki kupitia muziki,hivyo ameruhusu muziki kwenye kumbi za starehe mpaka saa 8 usiku,tunamshukuru sana kwa kuliona hilo"

Sanjari na hilo amewaomba mashabiki zake wampokee mtoto wake wa kike "brand" ambae anatarajia kuingia rasmi kwenye soko la muziki wa bongofleva .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...