Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Taifa Humphrey Polepole kulia akipokea tisheti ya umoja wetu ni ushindi wetu ya CCM kutoka kwa Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu kushoto wakati wa semina ya viongozi wa CCM wa Matawi na Kata iliyoandaliwa na CCM wilaya ya Tanga kwa kushirikiana Mbunge huyo katikati anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba
Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Taifa Humphrey Polepole wa pili kutoka kushoto akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo kulia ni katibu wa CCM wilaya ya Tanga Salim Kidima ambaye ameshikilia fedha zilizochangishwa kwenye semina hiyo kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba
MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto akiwa kwenye semina hiyo kulia ni Katibu wa CCM wilaya ya Tanga Salim Kidima akiwa anahesabu fedha zilizotolewa 
Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Taifa Humphrey Polepole akizungumza wakati wa semina ya viongozi wa CCM wa Matawi na Kata iliyoandaliwa na CCM wilaya ya Tanga kwa kushirikiana Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba akifuatiwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee 
Sehemu ya wanachama wa CCM wilaya ya Tanga wakifuaatilia kwa umakini hotuba ya Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Taifa Humphrey Polepole wakati wa semina ya viongozi wa CCM wa Matawi na Kata iliyoandaliwa na CCM wilaya ya Tanga kwa kushirikiana Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu

WANACHAMA wa chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tanga wametakiwa kujenga mshikamano na umoja miongoni mwao ili kuweza kuhakikisha wanakiwezesha chama hicho kupata ushindi kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani.

Hayo yalisemwa na Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Taifa Humphrey Polepole wakati wa semina ya viongozi wa CCM wa Matawi na Kata iliyoandaliwa na CCM wilaya ya Tanga kwa kushirikiana Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu.

Alisema lazima kuwepo mshikamano ambao utaawasaidia kuweza kuhakikisha wana kuwa wamoja kuelekea kwenye chaguzi zijazo ili kuhakikisha chama hicho kinaendelea kuwatumikia watanzania kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini.

Aidha pia katika semina hiyo Katibu huyo alifanya harambee kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya CCM wilaya ya Tanga ambapo jumla ya shilingi milioni 18 ziliweza kupatikana papo kwa papo huku Mbunge wa Viti Malumu (CCM) Mkoani Tanga ambaye pia Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akichangia shilingi milioni 5.

Sambamba na uchangiaji huyo lakini Waziri Ummy alitoa pia bendera za mashina 1000 na sare za chama ili kuimarisha chama ngazi za chini huku bendera 1000 za mabalozi na tisheti 800 ambazo watazitumia kwenye shughuli mbalimbali za kichama .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...