Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Prof.Sifuni Mchome akitia saini kitabu cha wageni kaoka Ofisi ya Katibu Tawala mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi aliekaa mbele akimuangalia.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Prof.Sifuni Mchome akiangalia Moja ya machapisho ambayo yapo katika KITUO Cha msaada wa sheria Singida alipokitembelea kituo kwa ukaguzi.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Prof.Sifuni Mchome akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa kituo cha msaada wa sheria Singida alipokitembelea kituo hicho kwa ukaguzi.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Prof.Sifuni Mchome akiwa katika picha ya pamoja na watoa huduma ya msaada wa sheria mkoani Singida alipokuwa mkoani humo kwa ziara ya ukaguzi.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Prof.Sifuni Mchome akizungumza na watendaji wa KITUO Cha msaada wa sheria Singida juu ya huduma za msaada wa sheria kwa wannachi alipofika kuangalia eneo wanalotumia kutoa msaada huo kwa wananchi.

*************************************************

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome atembelea mkoa wa Singida kukagua utoaji wa msaada wa kisheria kwa wananchi. Prof Mchome yuko katika ziara ya ukaguzi wa huduma na maeneo yanayotolewa msaada wa kisheria ili kuona kama inaendana na matakwa ya Sheria ya Msaada wa Kisheria No 1. ya 2017.

Katika ziara hiyo Prof. Mchome ambaye ameambatana na Msajili wa Watoa Msaada wa Kisheria nchini bibi Felistas Mushi, amezungumza na wanufaika wa huduma ya msaada wa kisheria katika mkoa wa Singida ambao wameelezea kuridhishwa kwako na huduma hiyo ambayo wamesema imewezesha kutatua matatizo yaliyokuwa yakiwakabili na hivyo kupata haki zao.

Ziara hiyo ya ukaguzi ni utekelezaji wa Sheria ya Msaada wa Kisheria No.1 ya 2017 ambayo inamtaka msimamizi wake kuvitembelea vituo vinavyotoa huduma ya msaada wa kisheria ili kuona maeneo wanakotolea huduma na aina ya huduma wanayoitoa kwa mujibu wa sheria hiyo.

Akizungumza na watoa msaada kutoka wilaya za Singida, Iramba, Mkalama Prof. Mchome amewataka kuzingatia kuwa msaada wa kisheria ni huduma muhimu ambayo wananchi wanahitaji kupewa kwa kuwa sio kila mwananchi anao ufahamu wa sheria.

Amewataka kuhakikisha wanatoa msaada wa kisheria ili kuwawezesha wananchi kutatua matatizo yanayowakabili na hivyo kuokoa muda ambao wangeutumia kujishughulisha kwa ajili ya maendeleoyao na taifa kwa ujumla.

Amesema matatizo mengi yanatatuliwa na sheria mbalimbali na ndio maana mtu akipata mtaalamu wa sheria anakuwa amepata njia sahihi na salama ya kutatua tatizo lake na kuokoa muda kwani atakuwa amerahisisha mambo mengi.

“Sheria ni kama uzio ambao una milango inayotakiwa kufunguliwa ili kuweza kujua njia sahihi ya kupita na kupitia msaada wa kisheria mtaweza kuwaonyesha njia sahihi wananchi wenye shida na hivyo kutatua matatizo yao,” alisema Prof. Mchome na kuongeza kuwa sheria zikitumiwa vizuri huleta jamii zenye amani na furaha nakufanya jamii hizo kupata maendeleo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...