Program Coordinator wa Agitos Foundation Bi Sheila Cleo
Mogalo ambaye aliwasili nchini siku ya
Jumanne 7 may 2019 jumamosi May 11, 2019 ametembelea mazoezi ya KUOGELEA
ya watu wenye ulemavu. Mazoezi ya watu
wenye ulemavu yamefanyika katika bwawa la kuogelea la shule ya Nordic iliyoko
Masaki, Dar es salaam. Bi Sheila alifuatana na Katibu Mkuu wa Tanzania
Paralympic Committee (TPC) Bwana Tuma Dandi katika kuangalia maendeleo ya
michezo ya watu wenye ulemavu.
Bi Sheila aliweza kuzungumza na Kocha Mkuu wa timu ya
Taifa ya watu wenye ulemavu ndugu Ramadhana Namkoveka jinsi anavyoendesha
mafunzo yake, anavyopata waogeleaji, kuwaandaa na changamoto mbalimbali
anazokutana nazo .
Ramadhan Namkoveka alimuarifu kuwa anapata
waogeleaji kutoka katika taasisi mbalimbali kama Watoto Kwanza ya Kawe, shule
za msingi na wengine ambao wanatoka katika mitaa. Mafunzo hayo ambayo anayatoa
bila gharama yoyote, alisema changamoto kubwa ni kupata bwawa la kuogelea
ambalo atapata nafasi ya kufanyia mafunzo.
Aidha Namkoveka ameshukuru uongozi
wa shule ya Nordic iliyoko Masaki Dar Es Salaam kuweza kuruhusu bwawa lake
kutumika na kuipa nafasi mchezo wa kuogelea hasa kwa watu wenye ulemavu.
Hakika
imeweza kuzalisha waogeleaji wapatao 14 wenye ulemavu mpaka hivi sasa ambapo mmojawao
Gerald Hamisi Sokolo ameweza kushiriki mashindano ya kimataifa kwa kushiriki
mashindano yaliyofanyika Nairobi Kenya tarehe 8-11 Februari 2018.
Gerald ni
mtanzania pekee kwa upande wa kuogelea kuweza kutambuliwa na Chama cha Kuogelea
cha dunia (World Para Swimming).Pia hivi sasa juhudi juhudi zinafanyika kuweza
kuwapeleka wachezaji katika mashindano ya kimataifa kabla ya mashindano ya
Paralympic yatakayofanyika Japan 2020.
Sheila amependa hali ya michezo kwa watu wenye ulemavu
ilivyo hapa nchini na akasema kuwa juhudi kubwa zinatakiwa zifanyike katika
awareness ili walemavu wengi waweze kushiriki katika michezo yote. Sheila ameondoka
siku ya Jumatatu tarehe 13 May 2019 na
kurudi Bonn Ujerumani ambako ndiko kwenye makao makuu ya Agitos Foundation
ambao ni washirika wakubwa wa International Paralympic Committee (IPC)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...