Mkuu wa Mkoa wa Mbeya akisaini kitabu maalumu kuashiria uzinduzi rasmi wa soko la Tumbaku Msimu wa 2018/19 Kimkoa katika Wilaya ya Chunya.
Mkuu wa Mkoa Mbeya Mh .Albert Chalamila akizugumza na wananchi wa Kijiji Cha Mtande Halmashauri ya Wilaya ya Chunya (Hawapo Pichani)Mara baada ya kuzindua soko la Tumbaku Msimu wa 2018/19, ambapo pia uliendana na uwekaji wa Jiwe la Msingi Chama cha Ushirika Cha Msingi Mtande Chunya 
Meckfason Moshi Mteuzi wa Tumbaku Mbeya na Iringa akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mbeya Mh .Albert Chalamila (Katikati) Mara baada ya kuzindua rasmi soko la Tumbaku msimu wa 2018/19 ,Kulia Mkuu wa Wilaya ya Chunya Merryprisca Mahundi.


SERIKALI Mkoani Mbeya imeyataka Makampuni ya ununuzi wa zao la tumbaku Wilayani Chunyani Mkoani Mbeya kuacha tabia ya kuwalalia wakulima wa zao hilo kwa kununua bei ndogo ambayo hainendani na gharana za uzalishaji.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Albert Chalamila wakati akizindua Soko la Tumbaku Kimkoa msimu wa 2018/2019 uzinduzi ambao umefanyika katika kijiji Cha Mtande Wilayani Chunya..

Amesema yapo baadhi ya makampuni ya ununuzi wa zao hilo la tumbuka yamekuwa yakiwalalia wakulima kwa kununua bei ndogo hasa kutokana na wakulima wengi kutokuwa na elimu pamoja uelewa mdogo kuhusu soko.

“inawezekana ndani ya makampuni hayo wapo wanaofaidika moja kwa moja wao binafsi na wala sio kuifadisha Kampuni wala wakulima kwa ujumla wake kwa makusudi huku wakijua kuwa ni uonezi kwa Mkulima ambapo unaweza kukuta hata watumishi wa serikali wapo .”Amesema 

Wakati huo huo Mkuu huyo wa Mkoa amekemea tabia ya baadhi ya wakulima kuuza tumbaku yao nje vyama vya ushirika kwasabau imekuwa mzigo kwa wanachama wengine kulipa madeni ya wakulima ambao wamekopa pembejeo za kilimo.

Pia ameitaka Kamati ya ulinzi na Usalama Halmashauri ya Wilaya Chunya pamoja na Chama cha Wakulima wa Tumbaku kuhakikisha inafnya msako wa wale wote wanajihusisha na tabia hiyo ya uuzaji wa tumbaku nje ya ushirika hata kama ni watumishi wa serikali.

Naye Mrajisi wa vyama vya ushirika Mkoa wa Mbeya Angel Maganga amesema changamoto kubwa ni Kuondoka kwa Makampuni mengi ambayo yaliingia Mkataba kwa ajili ya uzalishaji wa zao hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...