Anaadika Abdullatif Yunus, Michuzi Tv – Karagwe .

Wananchi na wakulima wa zao la Kahawa Mkoani Kagera wameombwa kufanya maandalizi mazuri, ikiwa ni pamoja na kuvuna kahawa iliyokomaa, kuikausha vizuri katika mazingira safi ili kuweza kupata daraja bora na bei bora katika Soko la Dunia.

Akizungumza na Wakulima pamoja na wadau wa Zao la hilo, katika uzinduzi wa msimu mpya wa Kahawa Wilayani Karagwe Mkoani Kagera, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti, amewataka wakulima kuzingatia sana vigezo vya Kahawa bora ili kupata bei nzuri sokoni, ambapo kama Mkoa kwa Msimu uliopita Kahawa iliyokusanywa ni Kilo Milioni 58.9 sawa na asilimia 50 ya Kahawa yote ya Tanzania.

Katika salaam zake Mhe. Gaguti ametoa angalizo na kusisitiza kwa wale wote wanaofikiria kufanya magendo ya Kahawa kwa kuuza Nchi jirani, kutojihusisha na magendo hayo na kukumbusha kuwa tayari Serikali inazidi kuweka mazingira mazuri ya Bei nzuri ya zao hilo itakayomnufaisha Mkulima na kuinua kipato chake na Taifa kwa ujumla.

Katika kuhakikisha suala la magendo linakomeshwa hasa kuanzia msimu huu ulioanza Mei Mosi, Mhe. Gaguti ameanzisha kampeni ya ukomeshwaji magendo hayo, ambapo kwa yeyote atakayesaidia kukamatwa kwa Magendo hayo, atapewa 30% ya mauzo ya kahawa hiyo mara baada ya kutaifishwa na Kikundi kitapewa 50% ya mauzo ya Kahawa itakayotaifishwa. 

Awali Mkuu huyo wa Mkoa Mhe. Gaguti amekutana na Menjimenti ya KDCU pamoja na Bodi ya KDCU na kuweka mustakabari wa pamoja katika kuelekea kuanza kukusanya kahawa hiyo ambapo Tarehe rasmi ya kuanza kukusanaya kahawa itatangazwa Rasmi mwezi ujao. 

Uzinduzi wa Msimu Mpya wa Kahawa umefanyika rasmi katika Kijiji cha Kituntu Wilayani Karagwe, Mei 23, 2019 katika Shamba la mfano la Mkulima wa Kituntu Ndg. Kajoki, ambapo kijiji cha Kituntu wamekuwa kinara wa uzalishaji Kahawa kwa Msimu uliopita.
 Mkuu wa Mkoa Kagera, Mhe. Gaguti akiwa shambani kwa Mkulima Bwana Kajoki alievaa (kofia), pamoja na Mkuu wa wilaya Karagwe Mhe. Godfrey Mheluka wakishikiria moja kati ya miche ya mibuni ya zao la Kahawa Kama ishara ya Uzinduzi rasmi wa msimu mpya wa Kahawa 2019 Mkoani Kagera.
 Pichani ni Kahawa inayoelekea katika hatua ya kukomaa tayari kuvunwa kwa ajili ya msimu mpya ulioanza Mei Mosi, kama ilivyokutwa shambani kwa Ndg. Mutawajjib Kajoki wa Kijiji cha Kituntu Wilayani Karagwe
 pichani ni RC Gaguti akizungumza na wananchi, wakulima na wadau wa Kahawa kijiji Kituntu kabla ya Uzinduzi wa Msimu mpya wa zao hilo la Kahawa Mkoani  Kagera

picha ya pamoja ya Mhe. RC Gaguti, Mkuu wa Wilaya Karagwe Mhe. Mheluka, Mwenyekiti wa CCM Karagwe Mhe. Mutafungwa pamoja na Menejimenti ya KDCU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...