* Akumbusha waajiri kuwaajiri walemavu kama sheria inavyosema

*Awapongeza wafanyakazi kwa juhudi wanazozifanya katika ujenzi wa taifa

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam  Paul Makonda amemuagiza Katibu tawala wa Mkoa na Wakurugenzi  wa Halmashauri zote jijini humo kuhakikisha wanawapandisha madaraja Watumishi wanaostahili ndani ya mwezi mmoja kuanzia leo.

 Makonda ametoa agizo hilo wakati wa maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi duniani (Mei Mosi) ambayo Mkoani humo yameadhimishwa katika uwanja wa uhuru jijini humo, amesema kinachomshangaza ni kuona wafanyakazi wanaostahili kupandishwa madaraja hawapandishwi licha ya kuwa na sifa na vigezo vinavyostahili.

Aidha  Makonda amewaagiza maafisa kazi kushughulikia kero za wafanyakazi kwa wakati ili watumishi wafanye kazi zao bila vikwazo.

Pamoja na hayo Makonda amewataka waajiri kuhakikisha watumishi wanafanya kazi katika mazingira bora na salama huku akiwakumbusha kuajiri walemavu kama sheria inavyowataka.

Hata hivyo   amehimiza watumishi kujituma katika kazi wanazofanya huku akiwapongeza walimu na watumishi wengine kwa juhudi za kushughulikia kero za wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  Paul Makonda akizungumza na wafanyakazi pamoja na wakazi wa Dar es salaam wakati wa maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi duniani Mei Mosi yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...