NA MWAMVUA MWINYI, CHALINZE 

MBUNGE wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete ametoa msaada wa vifaa mbalimbali ikiwemo mifuko ya saruji 20 na matofali 3,000 kwa ajili ya uanzishwaji ujenzi wa shule ya msingi katika kitongoji cha Choza .

Aidha amemkabidhi msaada wa baiskeli ya miguu mitatu (wheel Chair),mkazi wa Zomozi-Ubena mzee Cosmas Alphonce Chongwe ambae ni mlemavu wa miguu.

Katika hatua nyingine ,Ridhiwani alitoa fimbo nne maalum kwa ajili ya walemavu wa macho,kadi 23 za afya kwa ajili ya matibabu ya wazee, vyote vikiwa na thamani zaidi ya sh.milioni tano.

Mbunge huyo alitoa misaada hiyo baada ya kumaliza kikao chake alichofanya pamoja na wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Ubena-Zomozi.

Ridhiwani alieleza, msaada huo alioutoa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Ilani ya uchaguzi na maombi mbalimbali ya wananchi katika kata hiyo. 

Pamoja na hayo, alikutana na wanachama mbalimbali wa vikundi vya maendeleo katika kata hiyo, ambapo aliwahimiza kuendelea kujiunga vikundi ili kuweza kupata mikopo kirahisi na kuwezeshwa kuliko kuwa mmoja mmoja. 

Hakusita kusema, ataendelea kusaidia makundi maalum na kusimamia kero zinazowakabili wananchi wa jimbo la Chalinze. 
Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mh.Ridhiwani Kikwete akimkabidhi msaada wa Baiskeli ya Miguu mitatu (Wheel Chair),Mkazi wa Zomozi-Ubena Mzee Cosmas Alphonce Chongwe ambaye ni mlemavu wa miguu,leo baada ya Mbunge huyo kumaliza kikao chake alichofanya pamoja na Wajumbe wa Mkutano mkuu wa CCM wa Kata ya Ubena-Zomozi,Chalinze.Mh.Ridhiwani amekabidhi msaada wa vifaa mbalimbali ikiwemo mifuko ya saruji 20 kwa ajili ya uanzishwaji ujenzi wa shule ya Msingi katika kitongoji cha Choza,Matofali Elfu tatu,fimbo nne maalum kwa ajili ya walemavu wa macho,Kadi 23 za Afya kwa ajili ya matibabu ya wazee, vyote vikiwa na thamani zaidi ya shilingi Milioni tano
Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mh.Ridhiwani Kikwete akimuelekeza Mkazi wa Zomozi-Ubena Mzee Cosmas Alphonce Chongwe ,ambaye ni mlemavau wa Miguu namna ya kutumia Baiskeli ya Miguu mitatu (Wheel Chair),aliyomkabidhi kama msaada.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mh.Ridhiwani Kikwete akimkabidhi fimbo maalum kwa ajili ya walemavu wa macho,Josephat Mgonge,ambaye ni mlemavu wa macho
Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mh.Ridhiwani Kikwete akikabidhi mfuko wa saruji kwa uongozi wa chama cha CCM,ambapo Mh.Mbunge msaada wa mifuko ya saruji 20 na matofali 3,000 kwa ajili ya uanzishwaji ujenzi wa shule ya msingi katika kitongoji cha Choza .
Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mh.Ridhiwani Kikwete akikabidhi kadi ya matibabu maalum kwa Wazee,Mzee Ally Gola,ambapo kadi 25 zilitolewa kwa Wazee.
Mmoja wa Wazee akimshukuru Mbunge Ridhiwani Kikwete kwa kuwapatia msaada wa kadi za matibabu,kulia ni Diwani wa Kata ya Ubena-Zomozi,Nicholaus Muyuwa akishuhudia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...