JOSEPH MPANGALA
Serikali iko Mbioni Kujenga Kiwanda cha Mvinyo pamoja na
Juise kutokana na Mabibo ya korosho ambayo yamekuwa yakitupwa mara baada ya
korosho kuuzwa na hivyo Wakulima kukosa fedha za ziada kutokana na Tunda hilo.
Akiuliza swali la Nyongeza Katika Mkutano wa 15 kikao cha 29
Mbunge wa Ndanda Cecil Mwambe amehoji Utafiti uliokuwa ukifanywa na Chuo cha
Naliendele kilichopo Mtwara kuhusu Kochoko au mabibo ya Korosho umefikia wapi
Mpaka sasa kwa lengo la Kuwawezesha wakulima Kuweza kujinufaisha zaidi na zao
la korosho.
“Kochoko ni zile washi zinazotokana baada ya mavuno ya
korosho wakulima huwa wanazitupa na wengine huwa wanaziuza na wengine
wanatengeneza Gongo na inafahamika kwamba Gongo sio pombe haramu isipokuwa
namna inavyotengenezwa je Utafiti uliokuwa Ukifanywa na Chuo cha naliendele Umefikia
wapi”?
Akijibu swali hilo Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga amesema
kupitia Chuo cha Utafiti cha Naliendele tayari wamefanya Utafiti na kutoa
maagizo ya ujengwaji wa kinu ili kuweza kuzalisha Mvinyo pamoja na juisi
itakayotokana na mabibo kwa lengo la kuongeza thamani zao la Korosho.
“Ni kweli kabisa chuo chetu kupitia tawi letu la Naliendele
tumefanya utafiti wa kina na tumebaini kwamba kuna mazao mengi tunaoweza
kuzalisha kutokana na Korosho ikiwemo Juisi na ikiwemo mvinyo maalum unaotokana
na mabibo ya Korosho na tumetoa maagizo kwenye tawi letu sasa hivi kujenga kinu
cha kuweza kuchakata ili tuweze kuzalisha mvinyo pamoja na juisi ambayo
tutaiuza hapa Nchini na hivyo itaongeza thamani na mapato yatakayotokana na zao
la Korosho” amesema Hasunga Waziri wa Kilimo.
Mbunge wa Ndanda Cecil Mwambe
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...