Na Ahmed Mahmoud Arusha

Serikali imeeleza kuwa itatumia sekta ya utalii na watalii wanaokuja kutembelea nchini kushawishi uwekezaji mkubwa na kutangaza kufungua milango ya fursa ya uwekezaji nchini kwa lengo la kuinua uchumi na kuongeza fursa za ajira kwa vijana.

Hayo yameelezwa na Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Uwekezaji Angela Kairuki kwenye Kongamano la kuvutia wawekezaji lililofanyika Jijini hapa ambapo alibainisha mkakati huo wa serikali ya awamu ya tano kuongeza wigo mpana wa wawekezaji wakubwa kuvutiwa kuja kuwekeza nchini.

Amesema kuwa Tanzania itaendelea kupokea wageni wengi wanaokuja kwa ajili ya utalii na kuwatumia kutangaza fursa za utalii kama walivyofanya kwa wageni kutoka China ambao wapo nchini kwa siku nne kutembelea vivutio vya utalii ikiwemo Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro na Serengeti sanjari na Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara.

Amebainisha kuwa huu ni mkakati wa serikali ya awamu ya tano katika kupanua ushirikiano kwa lengo la kukuza biashara hususani ya madini na utalii kuongeza wigo wa mapato ya nchini na kutumia fursa ya rasilimali tulizojaaliwa

“Niombe ndugu zangu watanzania tuweze kuitangaza vizuri nchi yetu hususani nyinyi waandishi wa habari mmeona waandishi wenzenu kutoka China wanaitangaza nchi yetu hii itasaidia kuongeza watalii na kuitangaza Tanzania na rasilimali ilizonazo kwa manufaa ya sasa na baadae”

Awali akiongea kwenye kongamano hilo Naibu waziri wa nchi sera bunge ajira vijana na watu wenye ulemavu Anthony Mavunde ameishukuru wizara ya uwekezaji kwa kuja na mkakati huo wa kuongeza na kutangaza kuvutia uwekezaji nchini kwani anaona kupitia uwekezaji wataweza kupambana na changamoto ya mfumuko wa ongezeko la ajiri kwa vijana wanaomaliza vyuoni.

Amesema kuwa uwekezaji mkubwa utafungua fursa pana ya kuweza kuongeza wafanyakazi kwenye kada mbali mbali na sasa serikali kupitia watalii itafungua milango kwa wawekezaji wanaotaka kuja kuwekeza nchini kwani miongoni mwa watalii wengi wanaokuja wano fursa nzuri za kuwekeza nchini.

“Serikali inapenda wafanyakazi kutoka nje ya nchi kuja kufanyakazi nchini kwa kufuata sheria zilizopo na si kwamba inakataa wafanyakazi hao kwani wanaleta ujuzi mpya na kuongeza ufanisi kazini ila wafuate taratibu za kupata vibali tena sasa upatikanaji wake umeboreshwa”

Nae Mkurugenzi wa Taasisi ya uwekezaji nchini TIC Jofrey Mwambe amesema kuwa mpango wao ni kuweka mkakati wa kuongeza wawekezaji kuwekeza nchini na mkutano huo umeonyesha mafanikio makubwa kwa kampuni iliyowaleta wageni hao italeta wageni wengine mwaka huu takribani 10 elfu kutoka nchini China.

Amesema kuwa hiyo ni faida kwa watalii hao wanaokuja kutembelea vivutio vya utalii nasi tukaitumia nafasi hiyo kutangaza fursa za uwekezaji ikiwa ni mkakati wa kuongeza wigo wa uwekezaji nchini kusaidia kuinua pato la taifa.

Aidha kwa Mujibu wa Mkurugenzi wa taasisi ya sekta Binafsi Godfrey Simbeye amesema kuwa ujio wa wageni hao na wawekezaji kutoka taifa la China kwao ni faraja kwa ukuaji wa sekta binafsi kuongeza wigo wa pato la taifa na uchumi kwa ujumla.

Amesema uendeshaji wa uchumi ni muhimu sana kwani serikali ikiweka mazingira mazuri kwa kuvutia wawekezaji watanzania watapata mitaji kutokana na wawekezaji hao kuja kuweza ila serikali zao nazo ziliweka mazingira maziru ya kibiashara kwa wananchi wa mataifa hayo, “Tunaiomba serikali kuona umuhimu wa mazingira mazuri ya kuwekeza kwa wananchi wa Tanzania tunaishukuru serikali yetu ya awamu ya tano kuanza kuona umuhimu huo na kuiga mataifa kama ya wenzetu kutoka nje”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...