*Ni kuhusu unaokataza wakurugenzi kusimamia uchaguzi
*Yataka nakala halisi ya uamuzi, mwenendo wa shauri

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

OFISI ya Wakili Mkuu wa Serikali imewasilisha Mahakama ya Rufaa Tanzania notisi ya kukataa rufaa kupinga sehemu ya uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu kuhusu uamuzi wa mahakama hiyo katika kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Bob Chacha Wangwe dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na wenzake kupinga vifungu vya sheria ya Taifa ya Uchaguzi kuhusu wasimamizi wa uchaguzi.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali imesema pia pamoja na notisi hiyo Serikali imeomba kupatiwa nakala ya uamuzi na mwenendo wa shauri hiyo na kufafanua kutoka na taarifa hiyo ya Serikali uamuzi ambao umetolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania katika kesi hiyo hauna nguvu kisheria.

Akizungumza leo Mei 13,2019 jijini Dar es Salaam , kabla ya kutoa msimamo huo wa kukata rufaa kuhusu uamuzi huo wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Adelardus Kilangi ameeleza Mei 10 mwaka huu Mahakama hiyo Kanda ya Dar es Salaam ilitoa uamuzi kuhusu shauri la kikatiba Na 17 la mwaka 2018.

Ambalo lilifunguliwa na Bob Chacha Wangwe kupinga baadhi ya vifungu vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi ,sura ya 343 kama ilivyorekebishwa vinavyohusu uteuzi wa wasimamizi wa uchaguzi vinakinzana na Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 kama ilivyofanyiwa marekebisho.

Amesema uamuzi huo ulitolewa na jopo la majaji watatu ambao ni Jaji Dkt.Atuganile Ngwala, Jaji Dkt.Benhaji Masoud na Jaji Firimin Matogolo na kwamba shauri hilo lilifunguliwa chini ya Sheria ya utekelezaji wa haki za msingi na wajibu sura ya tatu ya sheria za Tanzania.

Ameongeza shauri hilo lilifunguliwa dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Mkurugenzi wa Uchaguzi. "Bob Chacha Wangwe ambaye alijitambulisha kama mpiga kura, alitaka Mahakama Kuu kuvitamka na kuvifuta baadhi ya vifungu sheria ya taifa ya uchaguzi kwa madai kuwa vinakinzana na ibara za Katiba."

Amevitaja vifungu hivyo ni kifungu cha 6(1) cha sheria ya taifa ya uchaguzi sura 343 kinachomtambua mkurugenzi wa uchaguzi ambaye ameteuliwa na Rais wa Tanzania kutoka katika utumishi wa umma.

Ambapo Mwanasheria Mkuu wa Serikali amefafanua mlalamikaji alitaka kifungu hicho kibatilishwe kwa madai kuwa kinakinzana na ibara ya 21(1), 21(2) na 26(1) ya Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977.

Pia wasimamizi wa uchaguzi, wakurugenzi hao hubanwa na masharti yanayosimamia uchaguzi chini ya sheria za uchaguzi. Katika utekelezaji wa jukumu la usimamizi, wakurugenzi hao huwajibika chini ya sheria ya sheria ya uchaguzi na si vinginevyo.

Kuhusu kifungu cha 7(2) , kinachotaka tume ya taifa ya uchaguzi, kuteuwa watumishi wa umma kusimamia chaguzi zinazoratibiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Serikali inaeleza kuwa hakikinzani na ibara ya 21(1) , 21(2) na 26(1) ya Katiba ya Tanzania.

"Zipo taratibu mbalimbali zinazozingatiwa wakati wakurugenzi hao na watumishi wengine wa umma wanapotakiwa kuhusika kusimamia uchaguzi ikiwemo viapo vya kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, umakini bila upendeleo,"amesema.

Akizugumzia kifungu cha 7(3), kinachoipa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mamlaka pale inapoona inafaa, kuteuwa wasimamizi wa uchaguzi kutoka miongoni mwa watumishi wa umma kuwa wasimamizi wa uchaguzi, Serikali ilieleza kuwa kifungu hichi hakikinzani na ibara hiyo ya 21(1),21(2) na 26(1) ya Katiba ya Tanzania.

"Utaratibu wa uteuzi wa watumishi wa umma kwenye uchaguzi, utazingatia sheria na kanuni za uchaguzi, na watumishi hao wanapotekeleza wajibu, wanazingatia sheria husika za uchaguzi,"amesema.


UAMUZI WA MAHAKAMA KUU

Akizungumzia uamuzi wa Mahakama hiyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema baada ya kusikiliza hoja za pande mbili ,Mahakama Kuu imeamua kwamba imeridhia uhalali wa Katiba wa kifungu cha 6(1) , sheria ya Taifa ya uchaguzi kinachomtambua Mkurugenzi wa Taifa wa uchaguzi ambaye anateuliwa na Rais kuendelea kusimamia chaguzi.

Pia imeridhia uhalali wa Kikatiba wa kifungu cha 7(2) cha sheria ya uchaguzi kinachoipatia mamlaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuteuwa wasimamizi wa uchaguzi kutoka miongoni mwa watumishi wa umma.

"Mahakama imethibitisha kifungu cha 7(1) na 7(3) vinavyowataka wakurugenzi wa majiji, halmashauri, miji na wakurugenzi wa wilaya pamoja na wateuliwa wa Tume ya uchaguzi kutoka katika utumishi wa umma kusimamia uchaguzi kwa kuwa vinakinzana na ibara ya 3.

"Kifungu cha 7(1) cha sheria ya taifa ya uchaguzi kinachowataka wakuregenzi wa majiji ,manispaa, miji na halmashauri za wilaya kusimamia chaguzi kwa madai kuwa kifungu hicho kinakinzana na ibara ya 21(1), 21(2) na 26(1) ya Katiba.Kifungu cha 7(2) kinachoitaka tume ya taifa ya uchaguzi kueteua watumishi a umma kusimamia chaguzi zinazoratibiwa na tume hiyo kwa madai kuwa zinakinzana na kuvunja haki ya msingi ya uhuru na wajibu unaolindwa na ibara ya 21(2), 21(2) na 26(1) ya Katiba,"amesema.

Pia amesema kifungu cha 7(3) kinachoipa Tume ya Taifa ya Uchaguzi mamlaka pale inapoona inafaa kuteua wasimamizi wa uchaguzi kutoka miongoni mwa watumishi wa umma kuwa wasimamizi wa uchaguzi.Badala ya wakurugenzi wanaotajwa na sheria kusimamia uchaguzi, na pale ambapo tume inawateua watumishi wa umma basi wakurugenzi tajwa wanakoma kuwa wasimamizi. "Mlalamikaji alipinga kifungu hiki kwa madai kuwa kinakinzana na ibara ya 21(1), 21(2) na 26(1) ya Katiba,"amesema.


KUHUSU UTETEZI WA SERIKALI

Amesema katika utetezi wake Serikali ilipinga madai hayo kwa kuwa hayakuwa na msingi.Kwenye maelezo ya utetezi, Serikali kupitia Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ilitao hoja kadhaa.

Ametaja hoja hizo kuwa kuhusu kifungu cha 6(1) cha sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura 343 kinachompa mamlaka Rais aliye madarakani kuteua mkurugenzi wa uchaguzi kutoka katika utumishi wa umma, Serikali ilieleza kifungu hicho hakikinzani na ibara ya 21(1) 21(2) nq 26(1) ya Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977.

Pia amesema Katiba ya Jamhuri ya Muungano na Sheria ya Taifa ya uchaguzi imeweka misingi na utaratibu wa uteuzi wa mkurugenzi wa uchaguzi na kuwa na mkurugenzi huyo atatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa masharti yaliyomo kwenye Katiba, sheria ya uchaguzi na kanuni zinazoongoza uchaguzi.

Kuhusu kifungu cha 7(1) cha sheria ya Taifa ya uchaguzi kinachowataka wakurugenzi wa majiji, manispaa, miji na halmashauri za wilaya kusimamia chaguzi kwa madai kifungu hicho kinakinzana na ibara ya 21(1), 21(2) na 26(1) ,Serikali ilienza kuwa Katiba kama sheria mama imetoa fursa kwa Bunge kutunga sheria mbalimbali na kwamba uteuzi wa mkurugenzi wa uchaguzi unaofanywa na Rais unazingatia sheria za nchi.

"Japokuwa wakurugenzi wanateuliwa na Rais aliyepo madarakani , wanapohusika kama 74(14) ya Katiba inayozuia anayehusika na uchaguzi kujiunga na Chama chochote cha siasa.

"Hivyo msimamo wa Serikali dhidi ya uamuzi ea Mahakama Kuu , ni kwamba baada ya uamuzi huo Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupitia Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, imenza taratibu za kisheria za kukata rufaa kwenda Mahakama ya Rufani Tanzania ili sehemu ya uamuzi huo upitiwe upya,"amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...