Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba (katikati) akizungumza na wazalishaji wa mifuko mbadala wa plastiki (hawapo pichani). Katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam, pamoja na mambo mengine wazalishaji hao wa mifuko mbadala wameihakikishia Serikali kuwa wako tayari kuongeza kasi ya usambazaji wa mifuko mbadala kote nchini. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Nchini Dkt. Samuel Gwamaka. Kulia Dkt. Freddy Manyika Kaimu Mkurugenz Idara ya Mazingira.
 Sehemu ya wazalishaji wa mifuko mbdala wa plastiki kutoka Kampuni mbalimbali wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa  Karimjee Jijini Dar es Salaam, pamoja na mambo mengine wazalishaji hao wa mifuko mbadala wameihakikishia Serikali kuwa wako tayari kuongeza kasi ya usambazaji wa mifuko mbadala kote nchini ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Serikali la kusitisha matumizi ya mifuko ya plastiki hapa nchini ifikapo tarehe 1 Juni 2019.

Bw. Heneriko Batamuzi kutoka Kampuni ya Kenwood Enterprise (T) Ltd akichangia mada katika kikao cha wadau cha kupitia Rasimu ya Kanuni  za kusimamia Taka Hatarishi hapa nchini. Ofisi ya Makamu wa Rais imeandaa rasimu ya Kanuni mpya za kusimamia Taka Hatarishi nchini ikiwa ni pamoja na ukusanyaji, urejelezaji, uteketezaji na usafirishaji wake ndani na nje ya nchi. Kikao hiki kimefanyika katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...