Shabiki wa Real Madrid ashinda Sh 208.5 milioni za M-Bet

Dar es Salaam. Mkazi wa Ifakara, mkoani Morogoro, Gadi Mwajeka (37) ambaye pia shabiki wa timu ya Real Madrid ameshinda kiasi cha Sh 208, 574, 790 baada ya kubashiri kwa usahihi mchezo wa Perfect 12 wa kampuni ya M-Bet.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi, Mwajeka alisema kuwa hakuamini mara baada ya kupigiwa simu kuambiwa kushinda kiasi kikubwa cha fedha.

Mwajeka ambaye ni mfanya biashara ya rangi za mkeka Ifakara mjini alisema kuwa ushindi huo ni faraja kubwa sana kwake kwani utamwezesha kuipanua biashara yake na kuanzisha nyingine.

“Sikuamini kama nimeshinda kiasi kikubwa cha fedha, nimetumia kiasi cha sh1,000 tu kubashiriki na kuingia kiasi kikubwa cha fedha. Nimefarijika sana,” alisema Mwajeka.

Alisema kuwa ameshiriki kubashiri muda mrefu mpaka kushinda kiasi kikubwa cha fedha. Alisema kuwa amecheza kwa miaka mitatu kucheza na hakukata tamaa.

“Mke wangu ni nesi, nilikuwa nachukua madaftari yake kuandika timu na kuanza kuzipigia mahesabu. Nitatumia fedha hizi kwa ushauri wa wazazi wangu kuona ninafanya biashara gani,” alisema.

Meneja Masoko wa Kampuni ya M-Bet, Allen Mushi kuwa Mwajeka ni mshindi wa tano tokea kuanza mwaka huu kushinda zawadi nono.

Mushi alisema kuwa M-Bet itaendelea kuwa nyumba ya mabingwa na kuwaomba mashabiki wa soka kubashiri na kampuni yao ili kuweza kubadili maisha.

“M-Bet ni nyumba za mabingwa na mabingwa wote wanapatikana kupitia michezo ya kubahatisha ya kampuni yetu na kujitajirisha vile vile vile kuichangia nchi yao kwani asilimia 20 ya fedha ukatwa kama kodi ya kusaidia maendeleo ya nchi katika sekta mbalimbali,” alisema Mushi.

Naye, Shabani Mwanga, Mkuu wa Kitengo cha Kodi za Michezo ya Kubahatisha (TRA), mkoa wa kodi wa Ilala alimpongeza Mwajeka kwa ushindi na pia kuipongeza kampuni ya M-Bet kwa kuwa walipa kodi wazuri kwa serikali.
Meneja Masoko wa kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi (Kulia) akimkabidhi mfano wa hundi mshindi wa droo ya Perfect 12, Gadi Mwajeka(Katikati) kutoka Ifakara, mkoani Morogoro aliyejishindia Sh 208.5 milioni baada ya kubashiri matokeo ya mechi 12 kwa usahihi. Kushoto ni Shabani Mwanga, Mkuu wa Kitengo cha Kodi za Michezo ya Kubahatisha (TRA), mkoa wa kodi wa Ilala.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...