Sheikh Hilaly Shaweji Makarani akiongoza dua baada ya kuongea machache juu ya mapenzi yake kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Na Said Mwishehe, Michuzi TV
I love you so much! Hivyo Sheikh Hilaly Shaweji Makarani almaarufu kama  Sheikh Kipozeo alivyomwambia Rais Dkt. John Pombe  Magufuli baada ya kukutana naye jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya Shirika la Simu Tanzania(TTCL) lilipokabidhi gawio kwa Serikali.

Sheikh Kipozeo amepata nafasi hiyo leo Mei 21, 2019 wakati alipopata nafasi ya kuomba dua kabla ya kuanza kwa tukio la utoaji gawio kwa Serikali kutoka Shirika la Simu Tanzania(TTCL) ambapo Rais Magufuli alikuwa mgeni rasmi.

Wakati anaitwa kusoma dua Mshereheshaji wa tukio hilo Tom Mushi ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TTCL amesema Sheikh huyo amekuwa akitamani kumuona Rais Magufuli kwa karibu.

Mushi alisema " Sheikh Kipozeo amekuwa akionekana mitandaoni mara kwa mara akisema anatamani siku moja aonane na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe  Magufuli kwani kuna jambo anataka kumueleza. Sheikh Kipozeo karibu umwambie Rais unachotaka kumwambia.",

Baada ya ukaribisho huo Sheikh Kipozeo alianza kwa kuomba dua na kisha akamwambia Rais Magufuli kwamba "I love you. Mimi ni Sheikh Hilaly Shaweji Makarani wa Rufiji huko, Na Rais wangu anatoka Mwanza.Narudia tene I love you so much...," amesema Sheikh huyo mbele ya Rais na umati mkubwa wa watu waliofika kwenye sherehe hizo.

Amesema anayo sababu kubwa ya kumpenda Rais Magufuli na mojawapo ni namna ambavyo Rais amekuwa mstari wa mbele katika kuleta maendeleo kwa ajili ya nchi yetu akitolea mfano ununuzi wa ndege nane. 

"Hatukuwa na ndege hata moja lakini Rais Magufuli amenunua ndege nane na binafsi nimezionja ,nimepanda kwenda Mwanza na kurudi na nimepanda kwenda Burundi.Tunakushukuru Rais kwa namna ambavyo unaitumikia nchi yetu kwa uzalendo mkubwa.

" Kazi yetu ni kuhakikisha tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu ili uwe na afya njema kuendelea kulitumia taifa letu la Tanzania,"amesema Sheikh Kipozeo na kusisitiza amefurahi sana kumuona Rais Magufuli kwa karibu zaidi kwani ilikuwa ni ndoto yake ya siku nyingi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...