SHIRIKISHO la Soka Duniani (FIFA) limekataa kuongeza idadi ya timu zitakazoshiriki kwenye michuano ya Kombe la Dunia ya 2022 itakayofanyika Qatar, kutoka timu 32 hadi 48 kama ambavyo ilikuwa imependekezwa.

Kwa mujibu wa FIFA imesema kuwa baada ya majadiliano ya kina na wadau wote muhimu sasa  imeamua kwamba chini ya mazingira ya sasa haitaweza kulitekeleza pendekezo hilo kwa wakati huu.

Hivyo michuano hiyo sasa itasalia na timu 32 za awali na hakutakuwa na pendekezo litakalowasilishwa kwenye kongamano lijalo la FIFA litakalofanyika Juni 5.

Uamuzi huo wa mwisho wa FIFA umetolewa mapema tofauti na ilivyotarajiwa kwamba yangetolewa wakati wa kongamano hilo litakalofanyika Paris nchini  Ufaransa kabla ya michuano ya Kombe la Dunia ya wanawake.

Rais wa FIFA, Gianni Infantino aliunga mkono pendekezo hilo, na maamuzi haya yanatajwa kuwa pigo kubwa kwake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...