Yapewa vifaa vya michezo vya zaidi ya shilingi laki tatu

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

SHULE ya msingi ya watu wenye mahitaji maalumu Buguruni viziwi inataraji kushiriki mashindano ya michezo ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu yanayoshirikisha shule za jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Afisa elimu Manispaa ya Ilala Elizabeth Thomas amesema kuwa wamejiandaa kutetea vikombe vyote katika ligi hiyo kwa watu wenye mahitaji maalumu, amesema kuwa wataingia kambini kwa siku 10 ili kupata timu ya Wilaya.

Amesema kuwa changamoto kubwa kwa sasa ni upungufu wa jezi, mipira pamoja na viatu na amewaomba wadau mbalimbali kujitokokeza na kuwasaidia watoto hao.

Kwa upande wake mkuu wa shule ya msingi Buguruni viziwi Mirembe Kurwa ameshukuru kwa msaada huo na kuahidi ushindi kwa Manispaa ya Ilala, na kusema kuwa wataendelea kushiriki michezo kupitia UMITASHUMTA kila mwaka.

Pia amesema kuwa watoto wenye ulemavu ni sawa na watoto wengine hivyo hatuna budi kuwalinda na kutetea haki zao pamoja na kuwafanya wajisikie kama watoto wengine.

Kwa upande wake meneja masoko Said Adinan kutoka X-TIGI mobile amesema kuwa wametoa zawadi chache ili kuweza kuwasaidia na kuwainua vijana hao kimichezo na kuwataka wadau wengine kuwaangalia watoto wenye mahitaji ya aina hiyo.

Adinan amesema kuwa wao kama ofisi wataangalia namna ya kuwasaidia watoto hao kwa kuanza na mshindi atakayeibuka katika mashindano hayo.
Mashindano hayo ya watoto wenye mahitaji maalumu yatashirikisha shule zote zenye mahitaji maalumu.
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Buguruni ya viziwi ,Milembe Kulwa akipokea vifaa michezo kutoka kwa  Meneja Masoko wa X-TIGI,Said Adinan vyenye thamani ya zaidi ya laki tatu leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Wanafunzi wa shule ya msingi Viziwi Buguruni wakionesha  Vipaji vyao vya kucheza mpira.
Picha ya pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...