KAMPUNI ya simu nchini, TECNO imedhamini mashindano ya wanafunzi wanaojifunza lugha na tamaduni za kichina katika chuo kikuu cha mlimani kwa kushirikiana na taasisi ya Confucius iliyopo chuoni hapo. 

Mashindano hayo yamefanyika katika ukumbi wa chuo uliopo katika jingo jipya la library iliyojengwa kwa udhamini wa watu wa china, yalishirikisha    takribani washiriki  kumi na mbili ambapo wote walikua ni wanafunzi  wa chuo kikuu cha mliman. 

Akizungumza wakati wa mashindano hayo meneja mahusiano, bwana Eric Mkomoye alisema kua  TECNO imesaidia kuwapa nafsi vijana  wa ktanzania  wanaotamni kutimiza ndoto zao kupitia kujifunza tamaduni za nchi nyingine  hasa katika kukuza  taaluma zao pia kuweza kuwasiliano na watu wa mataifa mbalimbali, aliendelea kwa kusema  kampuni yao  pamoja na  taasis ya Confucius wametoa zawadi mbalimbali ikiwemo  simu aina ya spark 3 pia safari ya kwenda nchii china kujifunza zaidi kw awashiriki washindi wawili. 

Mashindano ya kuongea kichina katika chuo kikuu cha mlimani hua yanfanyika kwa usimamizi mkubwa wa taasisi ya Confucius iliyoanzishwa mwaka 2013 kwa makubaliano kati ya chuo kikuu cha mlimani na makao makuu ya taasisi ya Confucius yaliyopo Hanban na Zhejiang yakihudhuriwa na makamu wa chuo kikuu cha mlimani  Prof. Rutinwa , mkuu wa utamaduni kutoka  ubalozi wa China bwana Gao Wei. 


Mwaka jana na mwka huu TECNO mobile imedhamini mashindano haya  na kuyaboresha kwa kuongeza zawadi kwa washindi, washiriki na hata wahudhuriaji  kwa njia  ya bahati nasibu, 

Kampuni ya TECNO kwa sasa inayotangaza simu yake mpya  aina ya TECNO Spark 3  imeeendlea kudhamini matukio mbalimbali yanayohusu  jamii  hasa katika kukuza vipaji vya vijana wa kitanzania na kufanikisha ndoto zao kupitia majukwaa mbalimbali ikiwemo ile maarufu ya kua shujaa wangu. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...