Na Joachim Mushi


MTANDAO wa Elimu Tanzania (TEN/MET) jana uliwasimamisha waandishi wa habari mbalimbali kwa dakika moja kabla ya kuanza mkutano nao, ikiwa ni ishara ya kumkumbuka Marehemu Dk. Reginald Mengi Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP ambaye amefariki dunia.


Akizungumza kabla ya tukio hilo, Mratibu wa Taifa wa TEN/MET, Bw. Ochola Wayoga alisema Marehemu Mengi alikuwa mmoja wa wadau wa elimu na amefanya mambo mengi kuchangia mafanikio ya sekta hiyo hivyo wanakila sababu ya kumkumbuka.

"...TEN/MET imeguswa na msiba wa Marehemu Dk. Mengi kwa kuwa alikuwa mdau mzuri katika kuchangia elimu, amefanya mambo mengi kuchangia na kusaidia wahitaji katika elimu...naomba tusimame kwa dakika moja kumkumbuka," aliwaambia wanahabari.

Jana  TEN/MET ilikutana na waandishi wa habari mbalimbali jijini Dar es Salam kuzungumzia shughuli za maadhimisho ya Juma la ELimu (GAWE) linalo tarajia kufanyika mkoani Tanga katika Wilaya ya Handeni.

Mratibu wa Taifa wa TEN/MET, Bw. Wayoga akizungumzia maadhimisho hayo alisema mwaka huu yataanza Mei 6 hadi 10, 2019 katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chanika, huku yakiambatana na mikutano vijiji mbalimbali kwa madhumuni ya kuhamasisha wanajamii kuhusu ushiriki wa pamoja na serikali katika kuboresha elimu iliyojumishi na endelevu.

"...Tarehe 10 Mei itakuwa ni kilele cha wiki ya uhamasishaji wa Elimu. Mgeni na mgeni wa Heshima atakuwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa. Kamati ya Maandalizi ya TEN/MET imeamua Kauli mbiu kwa Tanzania iwe ni: “ELimu Bora, Haki Yangu”.

Aidha alisema maadhimisho ya juma la elimu yatazinduliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Suleman Jafo mkoani Tanga yatakayofanyika  Wilayani Handeni.

"...Tarehe 10 Mei itakuwa ni kilele cha wiki ya uhamasishaji wa Elimu. Mgeni na mgeni wa Heshima atakuwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa. Kamati ya Maandalizi ya TEN/MET imeamua Kauli mbiu kwa Tanzania iwe ni: “ELimu Bora, Haki Yangu”. Alisema Mratibu huyo.
Mratibu wa Taifa wa TEN/MET, Bw. Ochola Wayoga (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumzia maadhimisho ya Juma la Elimu (GAWE) linalotarajia kufanyika katika Wilaya ya Handeni, Mkoani Tanga. Kulia ni Mwenyekiti wa GAWE, James Ogondick na Ofisa Utetezi TEN/MET, Bw. David Sizya (kushoto). 
Sehemu ya waandishi wa hahabari kulia wakiwa wamesimama kwa dakika moja kabla ya kuanza mkutano wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) na wanahabari kuzungumzia shughuli za maadhimisho ya Juma la ELimu (GAWE) linalo tarajia kufanyika mkoani Tanga katika Wilaya ya Handeni. 

Mratibu wa Taifa wa TEN/MET, Bw. Ochola Wayoga pamoja na meza kuu wakiwa wamesimama kwa dakika moja kabla ya kuanza mkutano wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) na wanahabari kuzungumzia shughuli za maadhimisho ya Juma la ELimu (GAWE) linalo tarajia kufanyika mkoani Tanga katika Wilaya ya Handeni. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...