RAIS wa Marekani Donald Trump amesema kwa sasa yuko tayari kufanya mzungumzo na viongozi wa Iran, kama watamtafuta. 

Trump amesema hayo leo Mei 10,2019 wakati anazungumza na waandishi wa habari katika Ikulu ya Marekani, ambapo amesema anatarajia viongozi wa Iran wampigie simu. 

Aidha Rais Trump amesema kwamba aliamuru kupelekwa kundi la manowari zinazobeba ndege za kivita katika Ghuba ya Mashariki ya Kati kwa sababu ya vitisho vya Iran. 

Mwaka jana, Trump alijiondoa kutoka mkataba wa nyuklia na Iran na kisha akaongeza vikwazo dhidi ya nchi hiyo. Umoja wa Ulaya umetoa wito wa kuwepo suluhisho la kidiplomasia kwa mzozo huo. 

Kwa siku ya jana viongozi wa jumuiya hiyo wakiongozwa na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel wamesisitiza kuhusu dhamira yao ya kuuheshimu muafaka huo wa mwaka wa 2015, lakini wakasisitiza kuwa hawatakubali masharti yoyote. 

CHANZO -DW 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...