TUME  ya Nguvu za Atomiki Tanzania(TAEC) imewashauri wafanyabiashara nchini kuendelea kupima bidhaa zao ili kuhakikisha mionzi yake ni salama na ambayo haitaleta madhara.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Profesa Busagala alipowasilisha mada katika mkutano wake na baadhi ya wafanyabiashara wa jijini Mwanza ambapo amesema kwa kupima bidhaa zao ni jambo la kufuata sheria.
 
 Pia amezungumza nao kuhusu majukumu ya tume kisheria ili kuongeza uelewa na kujadiliana hatua mbalimbali ambazo zitaisaidia kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara kwa wafanyabiashara wa Mkoa wa Mwanza na wafanyabiashara wote wanaolizunguka ziwa Victoria.
 
Katika mkutano huo ,wamejadili masuala mbali mbali ya Tume ya Atomiki Tanzania ikiwa ni pamoja na kuangalia mapungufu mbalimbali na hatimaye kuchukua hatua stahiki ili kuweka ustawi mzuri kati ya wafanyabiashara wa Mwanza na maeneo menginine nchini na kuyafanyia kazi kwa lengo la uboreshaji.

Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania ( TAEC) ambayo ndio mamlaka pekee yenye dhamana ya Udhibiti wa mionzi na uhamasishaji Salama wa matumizi ya teknolojia ya Nyuklia hapa nchini.

Hata hivyo katika mkutano huo Prof. Busagala amewaeleza wafanyabiashara hao kuwa athari za mionzi zinaweza kuleta madhara makubwa endapo kutakuwa na ukiukwaji wa kisheria
 
Prof. Busagala amesisitiza umakini na ushirikiano mkubwa unahitajika ili kuendelea kudhibiti na kuna ulazima mkubwa wa kupima bidhaa hizo ili kukidhi matakwa ya sheria ya Nguvu za Atomiki (Atomic Act No 7) na Sheria za Kimataifa kwani kwa kutokufanya hivyo kutakuwa na ukiukwaji sheria iliyopo ya udhibiti wa mionzi ili kutosababisha madhara yanayoweza kusababishwa na vimelea vya mionzi kwa wananchi na mazingira
 Wakiwa katika picha ya pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...