Mkuu wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora Gift Msuya akisisitiza umuhimu wa wananchi kutumia hati milki za kimila za kumiliki ardhi kujiletea maendeleo jana katika Kijiji cha Miyenze.
 Meneja Urasimishaji ardhi Vijijini kutoka Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanynge Tanzania(MKURABITA) Antony Temu akieleza faida za mafunzo kwa wakulima zaidi ya 100 wa Kijiji cha Miyenze Wilayani Uyui Mkoani Tabora wakati wa hafla ya kufungua mafunzo hayo jana katika Kijiji cha Miyenze.
 Kikundi cha Ngoma kutoka Kijiji cha Miyenze Wilayani Uyui mkoani Tabora kikitoa burudani wakati wa hafla ya kufungua mafunzo kwa wakulima wa Kijiji ya Miyenze yaliyoandaliwa na Kuratibiwa na Ofisi ya Rais MKURABITA ili kuwawezesha wakulima hao kuwa na kilimo chenye tija.
 Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya wazee maarufu wa kijiji cha Miyenze Wilayani humo jana baada ya kukabidhi hati 100 kwa wakazi wa eneo hilo.
 Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora Mhe Gift Msuya akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya wakulima waliopata hati miliki za kimila za kumiliki ardhi wa kijiji cha Miyenze Wilayani humo.
  Baadhi ya Wakazi wa Kijiji cha Miyenze wakimsikiliza jana Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya wakati wa hafla ya ugawaji wa hati za hakimiliki za kimila za ardhi kwa wakazi 100. PIX7. Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya akitoa hati ya hatimiliki ya kimila jana kwa Mkazi wa Kijiji cha Miyenzi Masele Makonda.
Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya akitoa hati ya hatimiliki ya kimila jana kwa Mkazi wa Kijiji cha Miyenzi Rufunga Maguki. Picha na WHUSM
NA TIGANYA VINCENT
WAKAZI wa Kijiji cha Miyenze wilayani Uyui wametakiwa kutumia hati za hakimiliki za kimila walizopewa kuomba mikopo kwa ajili ya uwekezaji katika kilimo na shughuli nyingine za kiuchumi ili kujiletea maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya wakati wa kufungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima wa Kijiji cha Miyenze na kukabidhi hati za hakimiliki ya ardhi za kimila kwa wakazi 100.

Alisema wakazi walipata hati za haki miliki hizo za kimila wanao usalama wa zao za ardhi na wameiongezea thamani ambayo inawafanya kuwa na fursa za kupata pesa.

Msuya aliongeza kuwa hati hizo zitawasaidia kupata dhamana hata kwenye vyombo vya kisheria kama vile Mahakama pindi wanatakiwa kuweka mali isiyo hamishika.

Alisema hati walizopata ni fursa pia ya kuwawezesha kuingia ubia na wawekezaji mbalimbali ambao wanatafuta ardhi inayotambulika kisheria kwa ajili ya kuwekeza katika sekta za viwanda, hoteli, maduka na shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka wakazi wa Kijiji hicho na maeneo mengine katika wilaya hiyo ambao mashamba yao hayajapimwa kuhakikisha wanaypima ili kuyaongezea thamani na kuwaondoa katika umaskini na kupunguza migogoro.

Alisema hakuna haja ya wananchi kukumbatia maeneo makubwa ambayo hayajapimwa kwa kuwa hayawezi kuwasaidia kupata maendeleo yao na nchi kwa ujumla kwa kuwa ni sawa na mali mfu.

Kwa upande wa Meneja Urasimishaji ardhi Vijijini kutoka Mpango wa kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanynge Tanzania(MKURABITA) Antony Temu alisema kuwa pamoja na kutoa hati hizo watawajengea uwezo wakulima 100 na viongozi 10 jinsi ya kuendesha kilimo bora na utunzaji wa kumbukumbu za hesabu za kilimo na biashara.

Alisema maeneo mengine ni jinsi ya kutafuta fursa na kuzitumia na ufugaji wa kuku wa kienyeji kibiashara na uandishiwa mpango wa biashara na uundaji wa vikundi vya uchumi.

Naye mmoja wa wakulima wa Kijiji cha Miyenze William Mauye aliishukuru Serikali kwa kuwawezesha kupima mashamba yao na hatimaye kuwapatia hati za haki miliki za kimila kwa kuwa zitawasaidia kuinua kipato chao kwa kuwa watakuwa na fursa ya kupata mikopo ya benki.

Alisema mkopo atakaochukua utamwezesha kununuza zana za kilimo za kisasa kwa ajili ya kuboresha kilicho chake cha mpunga na mahindi na hivyo kuongeza uzalishaji.

Mauye aliiomba Serikali kupitia MKURABITA kuendelea kuwasaidia wananchi wa vijiji ili wapimie ardhi yao na kuepuka baadhi ya watu ambao wakuwa wakichukua fedha zao bila hata kuwapimia maeneo yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...