Takwimu zinaonesha kuwa idadi ya wagonjwa wa Ugonjwa wa Dengue imeongezeka ambapo kwa sasa wamegundulika wagonjwa wapya 674 huku kata ya Ilala ikiongoza kwa kuwa na wagonjwa 235.

Akizungumza na waandishi wahabari Jijini Dar es Salaam Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Kambi amesema kuwa Ugonjwa wa Dengue kwa sasa wameongeza vituo kwa mkoa wa Dar es Salaam na Tanga hadi vituo 19 tofauti na awali ambapo vilikuwa 7.

Amezitaja  baadhi ya vituo vya Serikali vinavyopima Ugonjwa huo kuwa ni pamoja na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Amana, Temeke, Tumbi, Mkuranga  huku uhamasishaji wa upatikanaji wa vipimo zaidi vya Ugonjwa huo ukiendelea.

Aidha ameongeza kuwa dalili za ugonjwa huo ni pamoja na homa ya ghafla, Kuumwa kichwa hususani sehemu za macho, maumivu ya viungo na uchovu ambapo dalili hizo huanza kujitokeza kati ya siku 3 hadi 14 tangu siku mtu alipoambukizwa virusi vya Ugonjwa huo.

Sambamba na hayo amewakumbusha viongozi wa mikoa, Wilaya,  Halmashauri, Kata, Tarafa, Vijiji, mitaa na vitongoji  pamoja na Maafisa wa Afya nchini kuchukua hatua kwa dhati kwani Ugonjwa huo haupo ukanda wa Pwani tu bali unaweza ukatokea pia katika maeneo yao.

Hata hivyo amesema tangu kutokea kwa Ugonjwa huo January watu 1901 wamethibitishwa kuwa na virusi au walikwishapata ugua Ugonjwa huo ambapo kati ya hao 1809 wanatoka Dar es Salaam, 89 kutoka Tanga na mkoa wa Pwani, Singida na Kilimanjaro kukiripotiwa mgonjwa mmojammoja.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali Yudas Ndungile amesema wanaendelea na jitihada ya kuangamiza mazalia ya mbu ikiwemo kufukia kupulizia dawa  na wanamkakati wa kupata mashine ya kupuliza dawa angani.

Hata hivyo wito umetolewa kwa wananchi kwenda kupima pindi wanapoona dalili za ugonjwa huo na vipimo vinatolewa bure kwenye vituo vya Afya vya  Serikali huku akisisitiza kujikinga kwa kuangamiza  mazalia ya mbu kwa kufukia madimbwi, kufyeka vichaka na kuvaa nguo ndefu kwani mbu huyo hungata majira ya asubuhi mchana na jioni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...