Na Khadija Seif, Globu ya jamii.

UMOJA wa Wanawake Wajasiriamali ambao wanalea familia zao bila ya uwepo wa wanaume zao wameendelea kupewa mafunzo kwa lengo la kutambua changamoto ambazo wanakabiliana nazo bila kuwepo wenza wao.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa mafunzo hayo Mwenyekiti wa umoja huo Neema Steven amesema ni muhimu wanawake wakajitambua na kujua changamoto ambazo wanazikabili bila kuwepo kwa wenza wao na badae kutafuta suluhisho ili kusaidia familia zao pasipo kujihusisha na vitendo viovu kama kushiriki kwenye biashahara haramu ya ngono na wizi.

Amesema sababu nyingine ya kupatiwa mafunzo ya ujasiriamali wanawake hao pia ni kuwawezesha jinsi ya kujitambua,kujiari,kupatiwa mitaji kwa ajili ya kufanya biashara mbalimbali na kupatiwa masoko nje na ndani ya nchi kupitia biashara zao.

"Ni fursa sasa kwa wanawake nchi kote kujiunga na umoja huo ambao utaleta mabadiliko katika familia zao na Taifa kwa ujumla na kupunguza idadi ya omba omba barabarani na badala yake wanawake kujiari ili kupata fedha zitakazowawezesha kujikimu kiuchumi," amesema Steven.

Aidha, ameeleza tayari kwenye mafunzo hayo ya siku tano wanawake hao tayari wameshajiunga kwenye kikundi cha kupika chakula ambacho kitauzwa kwa bei nafuu na lengo ni kukusanya fedha hizo na kusaidia watoto yatima kwenye vituo mbalimbali nchini ambapo watu kutoka sehemu mbalimbali wameshaunga mkono jambo hilo.

" Tangu tumeanza mafunzo haya kuna wasanii wengi maarufu ambao wamekuja na baadhi yao ni Dayna, Madee na Dk.Cheni ambao wamelipia vyakula ikiwa ni mchango ambao umeingia kwenye mfuko wa kikundi,"amesema.

Kwa upande wake Msanii wa Bongo Fleva Sister Fay amesema pamoja na changamoto mbalimbali ambazo wanakutana nazo wanawake hao bado wameweza kutunza watoto bila ya uwepo wa baba wa watoto au waume zao.
Ametumia nafasi hiyo kuwataka wasanii kufika mahali kushiriki kwenye majukumu ya kijamii na sio kutoa burudani tu au kutaka kulipwa fedha katika shughuli za kijamii, bali watenge muda na kujitoa kwa hali na mali kusaidia jamii inayowazunguka. 
Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake wajasiAliamali hasa wanaotafuta ridhiki na kulea familia pasipo kupata msaada kutoka kwa mzazi mwenzie Neema Steven pamoja na mdau wa kikundi hicho ambae ni msanii wa bongofleva sister fey wakizungumza wakati wa mafunzo ya ujasiliamali kwa wanawake wanaolea familia zao bila kuwepo kwa mzazi mmoja (SINGLE MOTHER'S)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...