Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.
SHAHIDI wa pili katika kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa analichukia jeshi la polisi kuanzia siku alipoona video  kwenye mtandao wa kijamii wa you tube ikimuonyesha Zitto Kabwe  akielezea polisi wanavyowatendea ukatili raia.

Shahidi huyo Mashaka Juma ambaye ni msanii wa filamu, akiongozwa na Wakili wa serikali Mkuu Tumaini Kweka kutoa ushahidi wake, amedai, Oktoba 29,2018 huko Kimara Korogwe akiwa na wenzake wakicheza drafti alifika rafiki yao, Frenky Zong na kuwauliza kama wamepata habari yeyote ambapo wao hawakuwa na taarifa.

"Zong alitutolea simu yake kisha akatufungulia na tukaangalia habari kwenye yuotube ambapo tulimuona Zitto akililaumu jeshi la polisi kwa mambo mbalimbali ambayo wameyafanya wilayani Uvinza Mkoa wa Kigoma," amedai.

Ameendelea kudai kuwa,  kwenye video hiyo Zitto anaonekana akieleza jinsi jeshi la polisi linavyowanyanyasa wananchi, kuteka watu akiwemo  Mo wa Simba na jinsi walivyoenda hospitali kuwateka  watu waliokuwa wakitibiwa na kwenda kuwaua na pia video hiyo inamuonyesha Zitto akielezea jinsi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini alivyoshindwa kuwadhibiti askari wake .

Shahidi huyo amedai kuwa, alipoona video ile na taarifa aliyotoa Ziito ambaye anamfahamu kwa muda mrefu,  aliona jeshi la polisi halina thamani kama wameshindwa kulinda raia na mali zake ndipo alipolichukia hadi leo jeshi hilo.


Katika kesi , Zitto anakabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi anayodaiwa kutenda, Oktoba 28,2018 katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za  makao makuu ya chama cha ACT Wazalendo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...