Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), umekamilisha taratibu za kulichukua Shirikisho la Klabu za Waandishi wa Habari katika nchi za Afrika na Karibiani (African and Caribbean Press Club-ACP) ambapo makao makuu yake yatakuwa jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa UTPC Abubakar Karsan aliyasema hayo jana wakati akihitimisha mafunzo ya sheria mbalimbali za habari kwa waandishi wa habari wa Vyombo vya Habari Mbadala (Alternative Media) yaliyofanyika Morena Hoteli jijini Dodoma kwa siku mbili kuanzia Mei 21, 2019.

“Waambieni Watanzania jambo hilo.. .Waambieni watu wasioijua UTPC jambo hilo, waambieni watu wenye mashaka na UTPC jambo hilo, kwamba sasa tunaisimamia “Federation” (shirikisho) ya nchi zaidi ya 160” alisema Karsan akisisitiza kwamba hilo si jambo dogo bali ni hatua kubwa.

Aidha Karsan alitumia nafasi hiyo kushukru uwepo wa mradi wa DDA ambapo alisisitiza washiriki wake kutimiza wajibu wao ipasavyo ili kuhakikisha matarajio yanafikiwa na kuondokana na changamoto ya kutotimiza makubaliano jambo ambalo limekuwa likisababisha taasisi nyingi ikiwemo za waandishi wa habari kuvunjika.

Naye Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari (APC), Claude Gwandu alisisitiza kwamba klabu hiyo itahakikisha mradi huo unafanikiwa na kwamba haitasita kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayetaka kukwamisha mradi huo lengo likiwa ni kuleta mabadiliko katika jamii na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media) kupitia mradi wa utetezi na ushawishi wa haki za binadamu kwa kutumia takwimu (DDA), Midraji Ibrahim alisema mafunzo hayo yatawasaidia kupiga hatua katika majukumu yao ikiwa kila mmoja atafanyia kazi yale aliyojifunza huku akiishukru taasisi ya Freedom House kwa ushirikiano wake.

Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) unafadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo wa Watu wa Marekani kupitia taasisi za Freedom House pamoja na PACT kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka jana 2018 ambapo kwa waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media) unasimamiwa na UTPC kupitia APC.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wa Vyombo Vya Habari Mbadala (Alternative Media), wakinasa matukio jana jijini Dodoma wakati Mkurugenzi wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Abubakar Karsan akihitimisha mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi hao kuhusu sheria mbalimbali za habari ili kutekeleza kwa weledi mradi wa Utetezi na Ushawishi kwa kutumia Takwimu (Data Driven Advocacy-DDA), unaosimamiwa na UTPC kupitia Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Arusha (APC) kwa ufadhili wa taasisi ya Freedom House.
Picha na Kadama Malunde, Malunde 1 Blog
Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan akizungumza kwenye kwenye kilele cha mafunzo ya siku mbili kuanzia Mei 21-22, 2019 kwa waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Altenative Media) yaliyofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan aliwahimiza waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media) kutimiza wajibu wao ipasavyo ili kuhakikisha mategemeo ya mradi huo wa utetezi na ushawishi kwa kutumia takwimu yanatimia.
Wakili James Marenga ambaye alikuwa Mkufunzi wa Mafunzo hayo akitoa salamu zake.
Afisa Program kutoka UTPC, Victor Maleko akitoa ufafanuzi kwenye kilele cha mafunzo hayo.
Mwenyekiti wa waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media) kupitia mradi wa utetezi na ushawishi kwa kutumia takwimu (DDA), Midraji Ibrahim akitoa salamu zake kwenye kilele cha mafunzo hayo.
Mwenyekiti wa Arusha Press Club, Claude Gwandu akitoa salamu zake kwenye hitimisho la mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada kutoka kwa Wakili James Marenga.
Washiriki wa mafunzo hayo kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani wakiwa kwenye picha ya pamoja.

Tazama BMG Online TV hapa chini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...