Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV - Karagwe 

Katika kuelekea Fainali ya Mashindano ya Mpira wa Miguu yanayozishirikisha Timu 16 za waendesha Bodaboda kutoka vituo mbalimbali ndani ya Manispaa ya Bukoba, maarufu kama JPM BODABODA CUP 2019 KAGERA, Umoja Wa Vijana Karagwe Saccos (UVIKASA), umekabidhi zawadi ya mipira 16 kwa Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti ikiwa ni juhudi za kuunga mkono kazi nzuri inayofanywa na Mkuu huyo wa Mkoa wa Kagera katika kuwainua Vijana.

Zawadi hiyo imekabidhiwa Mapema Mei 23, 2019 na Mwenyekiti wa Saccos hiyo Yahya Salim Kateme, Kwa Mkuu wa Mkoa Mhe.Gaguti wakati alipofika katika Ofisi za UVIKASA kusalimia, akiwa katika ziara ya Kikazi Wilayani humor, ikiwa ni ahadi iliyotolewa na Mwenyekiti Yahya mapema baada ya kuanza kwa mashindano hayo, ambayo sasa yanaelekea ukingoni kwa michezo miwili iliyosalia ambayo ni mshindi wa tatu, na mchezo wa fainali, ambapo mipira hiyo itagawiwa kwa Timu zilizoshiriki.

Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa Mwenyekiti Yahya ameeleza kuwa Kama vijana wamekuwa wakiona juhudi za Mhe. Gaguti toka alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, kwa jinsi ambavyo amekuwa bega kwa bega kuhakikisha Vijana wanajikwamua Kiuchumi katika masuala mbalimbali, na hivyo kupitia Mashindano ya JPM BODABODA CUP, wameona ni vyema kuunga mkono kwa kutoa hicho kidogo kiongozwe katika zawadi za Timu zinazoshiriki Ligi hiyo.

Kwa upande wake Mhe. Gaguti katika shukrani zake ameahidi kuendelea kutoa Ushirikiano kwa SACCOS hiyo pale itakapokwama, na pia amefurahishwa na ubunifu wa Mwenyekiti huyo ambaye licha ya SACCOS hiyo inayoendelea kutoa Mikopo ya Riba nafuu kwa ajili ya kuinua vijana Wilayani Karagwe, pia tayari wamebuni miradi mingine ikiwemo ya Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji, Mbuzi na Ng’ombe, mradi wa mikopo ya Pikipiki kwa Vijana.
 Mwenyekiti wa UVIKASA Ndg. Yahya Salim akikabidhi Sare ya Umoja wa Vijana Karagwe Saccos, kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Gaguti, kama ishara ya Kumbukumbu ya ujio wake katika Ofisi hiyo.
 Mkuu wa Mkoa Kagera Mhe. Gaguti akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi za UVIKASA mjini Kayanga Wilayani Karagwe kwa ajili ya Kusalimia na Kuona Saccso hiyo hiyo inayojishughulisha na kuinua Uchumi wa Vijana Karagwe.
Pichani Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akipokea zawadi ya Mipira kutoka kwa Ndg. Yahya S. Kateme, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Karagwe Saccos (UIKASA) mara baada ya Kutembelea ofisi ya Saccos Hiyo, katikati ni Mkuu wa Wilaya Karagwe Mh. Godfrey Mheluka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...