*Miondoko yake haina tofauti na staili za Sam wa Ukweli

Na Ripota,Globu ya jamii

KADRI siku zinavyokwenda ndivyo sanaa ya muziki wa kizazi kipya hapa nchini unazidi kukua siku hadi siku huku vijana mbalimbali wakija kwa kasi na ubunifu wa hali ya juu katika utunzi wa mashairi yanayokonga nyoyo.

Miongoni mwa wasanii hao ni pamoja na Ronald Nnko ‘Ven Rossy’, mzaliwa wa Mkoa wa Arusha aliyeingia hivi karibuni katika sanaa ya muziki huo maarufu hapa nchini kama ‘Bongofleva’

Ven Rossy anayetamba na wimbo wake wa ‘Nakupenda’ ambao ndiyo uliomtambulisha kwa mara ya kwanza katika ulimwengu wa muziki nia yake ni kufika mbali kupitia sanaa hiyo hapa nchini na pengine Duniani kwa ujumla.

Akizungumzia ujio wake katika sanaa hiyo Ven Rossy anasema kwake muziki ni kitu kilichopo katika damu yake tangu akiwa mtoto akianza kuimba kwa kujifunza kupitia nyimbo mbalimbali walizokuwa wakiimba shuleni huku pia akifuatilia mashairi yaliyokuwa yakiimbwa na wasanii mbalimbali redioni

Ven Rossy ambaye unaweza kumfananisha na msanii Sam wa Ukweli ambaye kwa sasa ni marehemu, ujio wake katika sanaa hii ya muziki wa `BongoFleva’ ni kama vile utawafuta machozi mashabiki wa msanii huo kutokana na style ya uimbaji wake unaendana kwa kiasi kikubwa.

Anasema ujio wa ‘Nakupenda’ uliotengenezwa na Producer ‘Napoli’ kupitia Studio aliyoipa jina lake ‘Napoli’ ni kisa cha ukweli kinachohusu maisha yake ya uhusiano wa kimapenzi na msichana mmoja ambaye anakiri kuwa hakuwahi kupenda kama ilivyo kwa msichana huyo katika ulimwengu huu.

Ameimba mambo mengi katika wimbo huo uliotawaliwa na ufundi mzuri wa vinanda kutoka kwa ‘Napoli’ Producer aliyefanya makubwa katika sanaa ya muziki huo baada ya kufanya kazi mbalimbali zinazotamba katika vituo mbalimbali.

Video ya Nakupenda ambayo kama ilivyo kwa wimbo huo pia imeanza kutamba kupitia Channel ya ‘You-Tube’ na Televisheni mbalimbali hapa nchini imefanywa na Director ‘Diddy’ kiasi cha kuifanya video ‘kichupa’ hicho kuonekana kama moto wa kuotea mbali.

Anasema mbali na wimbo huo wa ‘Nakupenda’ kwa sasa yupo Studio akiendelea kurekodi nyimbo zingine mbili ambazo ujio wake utawahusisha ‘Corrabo’ wasanii mbalimbali wanaotamba katika sanaa hiyo.

Kuhusu wasanii waliopo katika sanaa hiyo ya muziki wa kizazi kipya Ven Rossy anasema wengi wanafanya vizuri hivyo anaamini atapata ushirikiano wa kutosha kutoka kwao na mashabiki wote wa muziki wakati huu ambao ameingia rasmi katika ‘Game’ hiyo.

Anasema hadi alipofikia ni kutokana na nguvu na jitihada zake binafsi akiwa hana Meneja kwa ajili ya kumsimamia huku akisisitiza kuwa yupo tayari kufanya kazi na Menegment yoyote itakayokuwa na malengo na dhamira ya kweli katika kazi.

Unaweza kumfollow Ven Rossy kupitia kurasa zake za Kijamii kwa account zifuatazo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...