NA Yeremias Ngerangera ,Namtumbo.

Askari 20 wanaosaidia kazi ya uhifadhi katika vijiji (VGS)hivi karibuni walipatiwa mafunzo ya ujasiliamali wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao pamoja na kuiendeleza jamii .

Mafunzo hayo yalikuwa ya siku nne yaliyolenga kuwapa ujuzi ,maarifa na stadi juu ya ujasiliamali ili kuwaepusha na vishawishi visivyo vya lazima na kujikita katika kazi zao pamoja na kujiongezea kipato.

Waliopata mafunzo hayo walikuwa 20 ambapo kati ya hao wasichana walikuwa 5na wavulana 15 huku mada za ujasiriamali zilizokuwa zinafundishwa zilikuwa kumi na tatu.

Chuo cha kijamii cha uhifadhi wa maliasili Likuyusekamaganga ndio eneo lililotumika kutolea mafunzo hayo huku Ofisi ya Maendeleo ya jamii katika Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo ndiyo iliyohusika kutoa mtaalamu wa kutoa mafunzo hayo.

Perez Kamugisha mkuu wa idara ya maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo alisema idara yake ilimteua Buyeke Rutaihwa kutoa mafunzo hayo ya siku nne kwa VGS hao.

Kamugisha alidai vijana waliopatiwa mafunzo ya siku nne ni vijana kutoka wilaya ya Chunya mkoa wa Mbeya ,Sikonge mkoa wa Tabora na Manyoni mkoa wa Singida.

Wakiongea kwa niaba ya VGS wenzao Lucy Moses na Ramadhani Issa walidai mafunzo hayo yamewasaidia kuwaongezea uelewa wa namna ya kuepuka vishawishi na namna ya kujikita katika ujasiriamali ili kujiongezea kipato katika jamii.

Hata hivyo VGS hao walimhakikishia mwendesha mafunzo hayo kuwa watazingatia mafunzo waliyopata kwa muda wa siku nne na kwenda kuyafanyia kazi yale yote waliyofundishwa ili kujiongezea kipato jamii zao na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake mwezeshaji wa mafunzo hayo Buyeke Rutaihwa kutoka katika idara ya Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo aliwapongeza VGS wote hasa kwa kufanya vizuri mitihani yao iliyotokana na mafunzo hayo na kufauri vizuri na kisha kuwataka kwenda kutumia mafunzo hayo waliyoyapata kwa vitendo ili kujiongezea kipato katika familia zao na jamii kwa ujumla aliwaambia Buyeke.

Katika Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo VGS wanapatikana katika jumuiya za uhifadhi (WMA)zilizopo katika Halmashauri ya wilaya Namtumbo ambazo ni Kimbanda,Kisungule na Mbarang”andu .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...