VIDEO ya wimbo mpya wa msanii maarufu nchini Amini Mwinyimkuu a.k.a Amini unaofahamika kwa jina la Nimenasa ambao amemshirikisha mwanadada Lina Sanga imeingia mtaani. 

Akipiga stori ya Michuzi Blog leo Mei 21, 2019 jijini Dar es Salaam Amini amesema video ya wimbo huo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa muziki wa kizazi kipya na sasa imekamilika kwani tayari ameiachia na iko mtaani na hasa katika mtandao wa youtube . 

"Video yangu mpya ya wimbo ya Nimenasa tayari imekamilia na leo ipo mtaani kwa maana ya link yake ipo mitandaoni.Ni video ambayo ina tofauti kubwa na video zangu za zamani kutokana na aina ya mazingira ambayo nimerekodia. 

"Katika kuhakikisha video yangu inakuwa tofauti nimeamua kwenda kurekodi katika hifadhi ya Msitu wa Magamba ambako ni tulivu na kuna mazingira mazuri. Hivyo kuna tofauti kubwa na mashabiki nimewapa kile ambacho walikuwa wanakihitaji kutoka kwangu,"asema Amini. 

Ametumia nafasi hiyo kufafanua ujumbe wake kwa Watanzania kwanza wahakikishe wanaiangalia video ya wimbo huo na kisha wajenge tabia ya kufanya utalii wa ndani kwani sehemu ya video ya Nimenasa amerekodi akiwa katika hifadhi ya msitu wa Magamba. 

Pia amesema hadi kufikia hatua ya kukamilika kwa video hiyo na kuiingiza mtaani, anatoa shukrani zake kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) kwani aliwaomba sehemu ya kwenda kurekodia na akukabuliwa."Nawashakuru kwani niliwafikia na wakanisaidia sana TFS."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...